?>

Iran yajibu baada ya Marekani kuiweka Answarullah katika orodha ya makundi ya kigaidi

Iran yajibu baada ya Marekani kuiweka Answarullah katika orodha ya makundi ya kigaidi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, kitendo cha serikali ya Marekani cha kuiingiza harakati ya wananchi ya Aswarullah katika orodha ya makundi ya kigaidi ni kukamilisha njama haribifu za vita vya kikatili na dhulma walivyobebeshwa wananchi wasio na ulinzi wa Yemen.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Saeed Khatibzadeh alitoa majibu hayo jana na kuongeza kuwa, tangu mwanzoni kabisa vya vita vya kivamizi vya Yemen, Marekani ilikuwa muungaji mkonono mkuu wa jinai za muungano wa Saudia Arabia na haijawahi kusita hata chembe kuwapa wavamizi hao misaada ya kifedha, kisilaha, kijasusi kimafunzo na kilojistiki.

Amesisitiza kwamba uamuzi wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani wa kuiingiza harakati hiyo ya wananchi ya Yemen katika orodha yake ya makundi ya kigaidi imeitia hofu jamii ya kimataifa na kuathiri pia juhudi za kuleta amani kwa njia ya mazungumzo, kama ambavyo imeathiri pia juhudi za kuwafikishia misaada wananchi wa Yemen waliosababishiwa maafa makubwa na uvamizi wa nchi yao. Aidha amesema, jamii ya kimataifa inapaswa kusimama imara kupinga na kulaani uamuzi huo wa kidhalimu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

Mike Pompeo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani mwenye chuki na Waislamu amesema kuwa, wizara hiyo imewasilisha kwa baraza la Congress, uamuzi wake wa kuliingiza jina la Answarullah katika orodha yake ya makundi ya kigaidi.

Uamuzi huo mpya wa Marekani umechukuliwa katika hali ambayo Saudia kwa kushirikiana na Imarati, Bahrain, Sudan na Misri, mwezi Machi 2015 zilianzisha mashambulio ya pande zote dhidi ya nchi maskini ya Kiislamu na Kiarabu ya Yemen. Tangu wakati huo hadi hivi sasa wavamizi hao wameizingira nchi hiyo kutokea angani, baharini na ardhi na kuzuia misaada isiwafikie raia wa kawaida waliowasababishia maafa makubwa kutokana na uvamizi wao.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*