?>

Iran yakamata tani moja na nusu ya mihadarati kusini mashariki mwa nchi

Iran yakamata tani moja na nusu ya mihadarati kusini mashariki mwa nchi

Kamanda wa jeshi la Polisi la Mkoa wa Sistan na Baluchistan wa kusini mashariki mwa Iran ametangaza kuwa, jeshi hilo limekamata karibu tani moja na nusu ya madawa ya kulevya kwenye eneo hilo.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Brigedia Jenerali Ahmad Taheri ametoa taarifa hiyo leo Jumatatu na kuongeza kuwa, maafisa wa polisi wa Iran wanaopambana na madawa ya kulevya katika mkoa wa "Sistan na Baluchistan" wako makini na wamefanikiwa kugundua genge moja lenye silaha linaloendesha magendo ya madawa ya kulevya kitaasisi na kulisambaratisha.

Licha ya vikwazo vikubwa na vya kila upande ilivyowekewa na madola ya kibeberu ya Magharibi kwa makumi ya miaka sasa, lakini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kugundua idadi kubwa sana ya madawa ya kulevya na kila mwaka huwa inagundua wastani wa tani elfu moja za madawa hayo haramu ambayo hupitishiwa nchini Iran kwa ajili ya kupelekwa katika nchi za Magharibi ambako ndiko hasa kuliko na wateja wakubwa wa madawa hayo haramu.

Jamhuri ysa Kiislamu ya Iran iko mstari wa mbele duniani katika vita dhidi ya mihadarati na hivi sasa maafisa wake wengine wameshauawa shahidi na kujeruhiwa. Takwimu zinaonesha kuwa Iran ina mashahidi na majeruhi zaidi ya 12,000 wa kupambana na magenge ya madawa ya kulevya. Hata Umoja wa Mataifa umekuwa ukilikiri suala hilo na umekuwa ukisema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiyo inayoongoza katika vita dhidi ya mihadarati kwenye ukanda huu.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*