?>

Iran yakosoa uamuzi wa kutoweka jina la Israel katika orodha ya wakiukaji wa haki za watoto

Iran yakosoa uamuzi wa kutoweka jina la Israel katika orodha ya wakiukaji wa haki za watoto

Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa kuunga mkono watoto hasa wasichana wanaojipata katika mapigano ya silaha ni msingi wa kimaadili na ubinaadamu huku akikosoa vikali uamuzi wa kutowekwa Israel na muungano vamizi wa Saudia katika orodha ya wanaokiuka haki za watoto.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Majid-Takht Ravanchi, Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameyasema hayo katika kikao cha Baraza la Usalama ambacho kilikuwa kinajadili maudhui ya: "Watoto katika mapigano ya kisilaha."

Mwanadiplomasia huyo wa Iran amekosoa vikali kimya cha Umoja wa Mataifa hasa Katibu Mkuu wa Umoja wa  Mataifa kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel na zile za muungano vamizi wa Saudia ambao unaendeleza vita dhidi ya Yemen. 

Ravanchi amesema ni jambo la kutia wasi wasi kuwa, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel hawajawahi kuorodheshwa katika ripoti za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kama wakiukaji wa haki za watoto. Aidha amebainisha masikitiko yake kuwa muungano vamizi wa Saudia nao pia umeondolewa katika orodha ya wakiukaji wa haki za watoto dunaini.

Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa  ametaka watoto wanaojipata katika mapigano ya kisilaha waungwe mkono na kuongeza kuwa hatua ya awali kabisa ni kuhitimisha mapigano yaliyoko maeneo mbali mbali duniani na kuzuia migogoro mipya kuibuka.

Aidha mwanadiplomasia huyo wa Iran amemkosoa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa kutozingatia kadhia ya namna vikwazo vya upande mmoja vinavyoathiri vibaya maisha ya watoto.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*