?>

Iran yalaani hujuma ya kigaidi dhidi ya jeshi la Misri

Iran yalaani hujuma ya kigaidi dhidi ya jeshi la Misri

Saeed Khatibzadeh, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani hujuma ya hivi karibuni ya kigaidi dhidi ya Jeshi la Misri katika Jangwa la Sinai ambapo wanajeshi kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Khatibzadeh amesema tatizo la ugaidi ambalo, kwa masikitiko makubwa limeenea katika nchi za Waislamu kwa uungaji mkono wa madola ya kigeni, linahitaji ushirikiano wa karibu wa nchi za eneo ili kukabiliana nalo.

Jeshi la Misri jana Jumamosi lilitangaza kuwa wanajeshi wake 10 na afisa wake mmoja wameuawa katika shambulio la kigaidi lililolenga mtambo wa kuchujia maji mashariki ya Mfereji wa Suez.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Misri, askari wengine watano wa jeshi hilo wamejeruhiwa katika operesheni ya kuwasaka na kuwaandama magaidi wa kundi hilo.

Kutokana na muundo wa idadi ya watu na mfumo wa kikabila wa watu wake; na vilevile kwa kuzingatia mazingira ya kijiografia ya mabonde na miinuko iliyoko kwenye Rasi ya Sinai, tangu mwaka 2011 na kuendelea, magaidi wameanzisha harakati zao katika eneo hilo; na baada ya kuibuka kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS), magaidi hao wametangaza kiapo cha utiifu kwa kundi hilo na kulipa genge lao jina la "Wilayat ya Sinai."

Ongezeko la ukosefu wa usalama na kushadidi hujuma za kigaidi Misri kumepelekea ongezeko la wananchi wengi ambao hawaridhishwi na utawala wa rais wa sasa wa nchi hiyo Abdul Fatah el Sisi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*