?>

Iran yamuonya mkuu wa IAEA asifanye 'mambo kuwa magumu'

Iran yamuonya mkuu wa IAEA asifanye 'mambo kuwa magumu'

Msemaji wa Shirika la Atomiki la Iran amemshauri Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) kujizuia kufanya mambo kuwa magumu kwa kutoa matamshi ya kisiasa.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Behrouz Kamalvandi ametoa onyo hilo Jumatano baada ya Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA kutoa wito kwa Iran kuanzisha mazungumzo haraka kuhusu kuhuisha mapatano ya nyuklia ya JCPOA ya mwaka 2015 kabla hali kuwa  ya 'matatizo zaidi'.

Katika kujibu, Kamalvandi amesema: "Namshauri Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA  ajiweke mbali na matamshi yasiyo ya kitaalamu yenye rangi ya kisiasa na yanayokusudiwa kwa vyombo vya habari."

Msemaji wa Shirika la Atomiki la Iran amesema iwapo kuna suala la kiufundi linapaswa kushughulikiwa kitaalamu katika fremu ya majukumu ya IAEA kupitia njia za kawaida za shirika hilo la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki.

Kamalvandi alikuwa akiashiria mahojiano ambayo Grossi aliyafanya hivi karibuni na televisheni ya CNN ya Marekani ambapo alitoa matamshi yenye uhasama usio wa kawaida dhidi ya Iran.

Grossi aliibua utata hivi karibuni alipofika katika utawala wa Kizayuni wa Israel na kukutana na wakuu wa utawala huo mwezi jana.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*