?>

Iran yataja sababu ya kuenea uhalifu na ugaidi kote duniani

Iran yataja sababu ya kuenea uhalifu na ugaidi kote duniani

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema sababu kuu ya kuenea uhalifu na ugaidi katika maeneo mbalimbali ya dunia ni magendo na biashara haramu ya silaha nyepesi na ndogo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Majid Takht-Ravanchi alisema hayo jana Jumatatu katia hotuba yake mbele ya Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wa Kutathmini Mpango wa Kimataifa wa UN wa Hatua Dhidi ya Magendo ya Binadamu.

Katika hotuba hiyo, Takht-Ravanchi ameeleza bayana kuwa, Jamhuri ya Kiislamu kama nchi nyingine duniani, ina wasi wasi mkubwa kuhusu matokeo mabaya ya kijamii, kiuchumi na kiusalama ya biashara haramu ya silaha ndogo ndogo; na namna silaha hizo zinavyowafikia kiwepesi watu wasiostahili.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran amebainisha kuwa, 'Mpango wa Hatua ya Kuzuia, Kupambana na Kuondoa Biashara Haramu ya Silaha Ndogo na Nyepesi Katika Viwango Vyote' ndiyo fremu pekee ya kimataifa inayokubalika ya kupambana na matatizo hayo.

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu kama mhanga wa ugaidi unaoungwa mkono na nchi ajinabi, uhalifu wa kupangwa, na magendo ya mihadarati na silaha ndogo ndogo, inathamini mpango huo wa kimataifa, na inatoa mwito wa kutekelezwa kwake kikamilifu kwa njia athirifu.

Amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liipigie darubini kadhia hii, sanjari na kuhakikisha kuwa biashara halali ya silaha hizo ndogo ndogo haiathiriwa. 342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*