?>

Iraq: Msimamo wetu ni kuunga mkono Palestina na kupinga kuanzishwa uhusiano na Israel

Iraq: Msimamo wetu ni kuunga mkono Palestina na kupinga kuanzishwa uhusiano na Israel

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iraq amesema kuwa, msimamo wa serikali ya nchi hiyo ni kuunga mkono taifa la Palestina na kwamba, Baghdad inataka taifa hilo madhulumu lirejeshewe haki zake zote zilizoporwa na kughusubiwa na utawala haramu wa Israel.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ahmed al-Sahafi amesisitiza kuwa, daima msimamo wa serikali ya Baghdad umekuwa ni kulinga mkono taifa la Palestina na kuhakikisha kuwa, wananchi hao madhulumu wanapatiwa haki zao.

Aidha msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iraq amebainisha kuwa, serikali ya Baghdad inasisitiza kwa mara nyingine kwamba, inapinga mwenendo wa kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Amesema: Misimamo ya serikali ya Iraq ni thabiti na daima imekuwa ikisisitiza kuwa, inaunga mkono taifa la Palestina na juhudi zote za wananchi hao za kupigania haki zao zilizoghusubiwa na Israel.

Kadhalika amesema kuwa, Fuad Hussein Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iraq amesisitiiza mara kadhaa katika mikutano ya kieneo na majukwaa ya kimataifa kuhusu kuunga mkono taifa hili haki ya taifa la Palestina na kupinga hatua yoyote ile ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Itakumbukwa kuwa, Septemba mwaka jana (2020), Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Imarati na Bahrain walisaini mkataba wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel katika hafla iliyofanyika Ikulu ya White House mjini Washington.

Baada ya hapo Sudan na Morocco nazo zikafuata mkumbo huo huo na kutangaza  kuanzisha uhusiano na utawala huo haramu, uamuzi ambao umeendelea kulalamikiwa na kulaaniwa na wapenda haki kote ulimwenguni

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*