?>

Ismail Hania: Muqawama ni njia fupi zaidi kwa ajili ya kurejesha haki za Wapalestina

Ismail Hania: Muqawama ni njia fupi zaidi kwa ajili ya kurejesha haki za Wapalestina

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ambaye amefanya ziara nchini Mauritania amesisitiza juu ya ulazima wa kuendeshwa muqawama ikiwa njia fupi zaidi ya kufanikisha kupatikana haki za Wapalestina zilizoporwa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ismail Hania ameeleza kuwa, chaguo la muqawama ni njia fupi zaidi kwa ajili ya kukomboa ardhi za Palestina na kurejesha haki walizoporwa Wapalestina. Hania ametamka hayo akiwa huko Nouakchott mji mkuu wa Mauritania. 

Jumatatu wiki hii Ismail Hania Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas aliwasili Mauritania akiwa katika ziara yake ya kiduru na kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Mohamed Ould Sheikh wa nchi hiyo. Hania amefuatana na ujumbe wa ngazi ya juu wa Hamas ziarani nchini humo. Mazungumzo kati ya ujumbe wa Hamas na Rais wa Mauritania yamefanyika katika ikulu ya rais huko Nouakchott hata hivyo ajenda ya mazungumzo kati ya pande mbili hizo haijawekwa wazi.  

Itakumbukwa kuwa, muqawama wa Palestina ulifanikiwa kujibu mashambulizi ya Wazayuni katika vita vya siku 12 huko Ukanda wa Ghaza kwa kutumia maelfu ya makombora na roketi za kisasa kabisa za wanamuqawama.   

Hatua hiyo ilililazimu baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni usiku wa Alhamisi ya tarehe 20 Mei mwaka huu kukubali kusimamisha vita huko Ghaza baada ya kushindwa kusitisha mashambulizi ya makombora ya makundi ya muqawama. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*