?>

Ismail Haniyeh: Damu ya mashahidi wa Jenin haitapotea bure

Ismail Haniyeh: Damu ya mashahidi wa Jenin haitapotea bure

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kwamba damu za mashahidi waliouawa na utawala haramu wa Israel katika eneo la Jenin hazitapotea bure. Ismail Haniyeh ameyasema hayo akizungumzia jinai ya Wazayuni ya kuwaua shahidi vijana watatu wa Kipalestina huko Jenin.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Mapema Ijumaa iliyopita askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel walivamia gari la Wapalestina lililokuwa limebeba vijana watatu na kuwaua shahidi kwa kuwamiminia risasi.

Akizungumza kwa njia ya simu na familia za mashahidi hao wa Kipalestina, Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amelaani mauaji ya vijana hao na kuongeza kuwa, Wazayuni walifanya jinai hiyo kwa kufuata njama iliyopangwa hapo kabla. 

Haniyeh ameeleza kuwa, jinai hiyo ya kuwauwa vijana watatu wa Kipalestina ilifanyika katika mwendelezo wa jinai mbalimbali za utawala huo dhidi ya wananchi wa Palestina.

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas ameeleza kuwa, mashahidi wa Kipalestina siku zote wanasonga mbele katika upande wa kuihami Palestina, Quds na Msikiti wa Al-Aqsa na wamechagua njia ya mapambano. Ameongeza kuwa, njia ya mashahidi hao itaendelezwa.

Duru za hospitali katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu zimewataja vijana waliouawa kwa kumiminiwa risasi na askari wa Israel kuwa Youssef Nasser Salah, 23, Baraa Kamal Lahlouh, 24, na Laith Salah Abu Srour, 24. 

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, Wapalestina zaidi ya 70 wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2022.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*