?>

Israel haiwezi kukana kuwa ndiye nduli wa Sabra na Shatila

Israel haiwezi kukana kuwa ndiye nduli wa Sabra na Shatila

Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limechapisha ripoti maalumu inayothibitisha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ndiye nduli wa mauaji ya umati ya Wapalestina katika kambi za wakimbizi za Sabra na Shatila za nchini Lebanon.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Kuanzia tarehe 16 hadi 18 "Septemba 1982, utawala wa Kizayuni wa Israel ukiongozwa na nduli Ariel Sharun ambaye alikuwa waziri wa vita wa wakati huo wa utawala huo katili, kwa kushirikiana na wanamgambo wa Kikristo wa Phalang wa Lebanon walifanya mauaji makubwa ya umati na ya kikatili dhidi ya raia wasio na ulinzi wa Palestina katika kambi za wakimbizi za Sabra na Shatila mjini Beirut.

Televisheni ya al Manar imelinukuu gazeti hilo la Kizayuni likisema kwenye ripoti yake kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel ndiye muhusika mkuu wa jinai hizo za Sabra na Shatila za mwaka 1982. 

Ripoti hiyo ya gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth imesema pia kuwa, majenerali na maafisa wa kijeshi wa utawala wa Kizayuni kwa kushirikiana na Bashir Gemayel, mkuu wa chama hicho cha Phalang ambacho kinajulikana pia kwa jina la Kataeb, ndio waliofanya jinai hiyo ya kutisha.

Katika mauaji hayo ya kigaidi na ya kinyama, wanajeshi makatili wa Israel waliwaua kwa umati watoto wachanga na wadogo pamoja na wanawake wa Kipalestina wasipungua 3,297 katika kambi hizo za Sabra na Shatila za mjini Beirut, Lebanon mwaka huo wa 1982. 

Watu wote waliouawa kwa umati kwenye jinai hiyo ambao walikuwa ni Wapalestina na Walebanon, walifikia 20,elfu. 136 kati yao walikuwa ni Walebanon. Miili 1,800 ya wahanga hao ilitelekezwa kwenye vichochoro vya kambi hizo mbili za Wapalestina. Wapalestina 1,097 walikufa shahidi kwenye hospitali ya Ghaza na 400 wengine walikufa shahidi kwenye hospitai ya Akka.342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*