?>

Israel imebomoa makumi ya majengo ya Wapalestina mjini Quds

Israel imebomoa makumi ya majengo ya Wapalestina mjini Quds

Shirika huru la kutetea haki za binadamu limesema utawala wa Kizayuni wa Israel umebomoa majengo 58 ya Wapalestina katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) tokea mwanzoni mwa mwaka huu hadi sasa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika taarifa ya jana Jumatatu, shirika la Euro-Mediterranean Human Rights Monitor limesema katika kipindi cha miezi minne iliyopita, Israel kwa upande mmoja imeshadidisha ubomoaji wa nyumba na majengo ya Wapalestina katika mji wa Quds tukufu, na kwa upande mwingine imejenga maelfu ya nyumba za walowezi wa Kizayuni katika maeneo hayo ya Wapalestina yanayokaliwa kwa mabavu.

Taarifa ya shirika hilo lenye makao yake mjini Geneva imeongeza kuwa, tokea Januari mwaka huu hadi sasa, Tel Aviv imeidhinisha ujenzi wa vitongoji karibu 5,000 vya walowezi wa Kizayuni mashariki mwa mji huo mtukufu.

Shirika hilo limeeleza bayana katika taarifa yake kuwa, lengo la ubomozi wa nyumba za Wapalestina na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ni kufuta uwepo wa Waarabu wa Kipalestina katika mji huo mtukufu.

Shirika la Euro-Mediterranean Human Rights Monitor limetaja vitendo hivyo vya utawala haramu wa Israel kama hatua za kibaguzi zinazokusudia kuondoa kikamilifu athari za Wapalestina na maeneo yao matakatifu.

Tariq al-Lewa, Afisa Mkuu wa Sheria wa shirika hilo la kutetea haki za binadamu amesema uamuzi wa Israel wa kubomoa na kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina unaonesha wazi namna utawala wa Kizayuni umejengeka katika mfumo wa ubaguzi aina ya Apartheid.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*