?>

Israel inapanua kwa siri kituo chake cha silaha za nyuklia

Israel inapanua kwa siri kituo chake cha silaha za nyuklia

Picha mpya za satalaiti zinaonyesha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel, ambao ni mmiliki pekee wa silaha za nyuklia Asia Magharibi, unatekeleza mradi wa kupanua kituo chake cha siri cha nyuklia katika Jangwa la Negev.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Picha za satalaiti zinaonyesha ujenzi mkubwa ukiendelea katika kituo cha nyuklia cha Dimona. Ujenzi huo umethibitishwa na taasisi ya kimataifa ya masuala ya mada za nyuklia, IPFM, ambayo inajumuisha wataalamu kutoka nchi 17.

IPFM imesema ujenzi unaendelea katika maeneo kadhaa  karibu na tanuri nyuklia.

Akizungumza na gazeti la The Guardian, Pavel Podvig, mtaalamu wa masuala ya nyuklia na usalama wa kimataifa katika Chuo Kikuu cha Princeton amesema ujenzi huo ulianza mwishoni mwa mwaka 2018 au mapema 2019.

Utawala haramu wa Israel umekataa kutoa taarifa kuhusu mradi wake wa silaha za nyuklia. Kwa mujibu wa Jumuiya ya Wanasayansi wa Marekani, Israel inakadiriwa kuwa na vichwa 90 vya silaha za nyuklia. Silaha hizo zimeundwa kwa kutumia mada ya plutonium ambayo imepatikana katika tanuri nyuklia ya maji mazito ya Dimona.  Kituo cha Dimona kinaaminika kuwa muhimu kwa mradi wa Israel wa kuunda silaha za nyuklia.

Utawala haramu wa Israel umepuuzilia mbali miito ya kuweka wazi vituo vyake vya nyuklia ili vikaguliwe na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki. Ukaidi huo wa Israel unatokana na uungaji mkono wa Marekani.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni