?>

Israel yakataa kuwapatia chanjo ya corona mateka Wapalestina inaowashikilia katika jela zake

Israel yakataa kuwapatia chanjo ya corona mateka Wapalestina inaowashikilia katika jela zake

Utawala haramu wa Kizayuni wa Israel unakataa kuwapatia chanjo ya corona mateka Wapalestina unaowashikilia kwenye magereza yake.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Idara ya habari inayohusika na masuala ya mateka Wapalestina imetangaza kuwa, waziri wa usalama wa ndani wa utawala wa Kizayuni anashikilia kwamba, mateka Wapalestina wa masuala ya usalama wasipigwe chanjo ya corona na kwamba chanjo hiyo itolewe kwa wafanyakazi tu wa magereza wanakoshikiliwa Wapalestina hao, uamuzi ambao unahalifu taratibu na hati za kimataifa.

Idara hiyo ya habari inayohusika na masuala ya mateka Wapalestina imetahadharisha kuhusu hatari inayowakabili mateka Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye jela za utawala haramu wa Israel na kusisitiza kuwa, kubainika kesi nyingine mpya za watu walioambukizwa virusi vya corona katika kitengo cha nne cha jela ya Raymun kunaashiria hatari kubwa sana inayowakabili mateka hao.

Taarifa iliyotolewa na idara hiyo imezitaka taasisi husika za kimataifa kutekeleza jukumu lao kuhusiana na jinai na ukiukaji sheria unaofanywa na utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa kamati inayoshughulikilia masuala ya mateka Wapalestina, idadi ya Wapalestina walioambukizwa virusi vya corona katika magereza ya utawala wa Kizayuni imefika watu 191...

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*