?>

Italia: Chanjo wa corona ya Russia ni nzuri na ni salama

Italia: Chanjo wa corona ya Russia ni nzuri na ni salama

Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Kuambukiza ya Italia imetangaza kuwa, chanjo ya ugonjwa wa COVID-19 iliyotengenezwa nchini Russia ambayo inajulikana kwa jina la "Sputnik V" ni nzuri na ni salama.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Taasisi hiyo imesema, utendaji kazi na usalama wa chanjo ya "Sputnik V" katika kukabiliana na corona, unaweza kuwekwa daraja sawa na chanjo za Pfizer na Moderna. 

Huku hayo yakiripotiwa, taarifa nyingine zinasema kuwa karibu Waitaliano laki saba wamepoteza kazi zao katika kipindi cha baina ya mwezi Novemba 2019 hadi Novemba 2020 kutokana na wimbi kubwa la maambukizi ya kirusi cha corona na madhara yake kwa uchumi wa nchi hiyo.

Kuporomoka nafasi za ajira nchini Italia kulikotokana na kuenea ugonjwa wa corona kumewaathiri watu wengi hasa wafanyakazi wa mikataba yenye muda maalumu.

Takwimu zinaonesha kuwa, katika kipindi cha miezai 11 ya mwanzoni mwa mwaka 2020, watu milioni 4 na laki saba na 55,000 waliajiriwa nchini humo, kiwango ambacho kinaonesha upungufu wa asilimia 30 ya ajira ikilinganishwa na muda kama huo mwaka 2019.

Aidha takwimu zinaonesha kuwa, idadi ya maambukizo ya corona yameongezeka katika maeneo tofauti nchini Italia. Kulingana na vipimo vinavyotolewa vya wastani wa watu laki moja, wiki iliyopita idadi ya maambukizo iliongezeka hadi watu 135 wakati wiki za huko nyuma, idadi ya maambukizo ilikuwa chini ya hiyo kwa kila watu laki moja.

Italia ni ya nne kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa COVID-19 barani Ulaya baada ya Uingereza, Ufaransa na Uhispania.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni