?>

Jacob Zuma ataka kuakhirishwa kesi yake ya ufisadi

Jacob Zuma ataka kuakhirishwa kesi yake ya ufisadi

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ambaye kuwekwa kwake kizuizini mapema mwezi huu kumezusha machafuko mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo baada ya kumalizika kipindi cha ubaguzi wa rangi, ametuma ujumbe kwa njia ya video akitaka kuakhirishwa kesi yake ya ufisadi kuhusu mkataba wa silaha.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sasa hivi Serikali ya Afrika Kusini imefanikiwa kudhibiti machafuko katika maeneo mengi ya nchi hiyo. Hata hivyo kuna hofu kwamba iwapo Jacob Zuma ataonekana tena mahakamani, basi huenda kukazuka fujo nyingine kubwa nchini humo. 

Juhudi za kumpandisha kizimbani rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini kwa tuhuma za ufisadi wa dola bilioni 2 katika mkataba wa silaha wa miaka ya 1990 zinahesabiwa kuwa ni moja ya mitihani mizito ya nchi kwa ajili ya kuonesha uwezo wake wa kuwapandisha kizimbani wanasiasa wenye nguvu na ushawishi mkubwa.

Zuma amekanusha tuhuma za kuhusika katika ufisadi huo na kusema kuwa yeye ni muhanga wa malengo maovu ya baadhi ya wanasiasa ambao walikusudia kumuharibia jina na kumporomosha kisiasa kwa miaka mingi. 

Wiki iliyopita Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini iliagiza Rais mstaafu wa nchi hiyo, Jacob Zuma afungwe jela kwa kukataa kutoa ushahidi katika uchunguzi wa ufisadi uliofanyika wakati wa uongozi wake kuanzia mwaka 2009 hadi 2018. 

Miji mingi ya Afrika Kusini imeshuhudia machafuko mabaya zaidi kuwahi utokea nchini humo tangu baada ya kuondolewa utawala wa makaburu mwezi Mei 1994 alipoingia madarakani hayati Nelson Mandela.  

Hata hivyo, jana Jumatatu, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini alisema kuwa, utulivu umerejea katika aghlabu ya miji ya nchi hiyo, ingawa alisema pia kuwa, uharibifu na uporaji uliofanyika ni mkubwa mno na unaweza kufikia mabilioni ya rand, sarafu ya nchi hiyo.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*