?>

Jenerali Salami: Uchokozi wowote wa adui dhidi ya Iran utakabiliwa na jibu kali

Jenerali Salami: Uchokozi wowote wa adui dhidi ya Iran utakabiliwa na jibu kali

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema damu ya Shahidi Hassan Sayyad Khodaei haitamwagika bure na kusisitiza kuwa, hatua na uchokozi wowote wa adui utakabiliwa na jibu kali.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mlinzi wa Haram, Kanali Hassan Sayyad Khodaei aliuawa shahidi Jumapili mjini Tehran katika hujuma ya kigaidi ya wapinga Mapinduzi ya Kiislamu na maajenti wa madola ya kiistikbari duniani.

Mazishi ya Shahid Hassan Sayyad Khodaei yamefanyika leo mjini Tehran na kuhudhuria na halaiki kubwa ya watu katika Medani ya Imam Hussein AS.

Akizungumza na Kanali ya Televisheni ya Al Masirah, Brigedia Jenerali Hussein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema damu ya Shahidi Khodaei haitamwagika bure na kwamba jibu kali litatolewa kuhusu jinai hiyo.

Brigedia Jenerali Salami amesema Iran haitamuacha adui abakie hivi hivi na kwamba uchokozi wa adui utakabiliwa na jibu kali

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*