?>

Jeshi la Iran la IRGC lafanya mazoezi makubwa zaidi ya nchi kavu

Jeshi la Iran la IRGC lafanya mazoezi makubwa zaidi ya nchi kavu

Kikosi cha Nchi Kavu la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limefanya mazoezi makubwa zaidi ya pamoja ya kijeshi kusini mashariki mwa nchi .

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mazoezi hayo ya kijeshi yaliyopewa jina la Muhammad Rasulullah SAW yamefanyika Alhamisi katika mkoa wa Sistan na Baluchestan.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim, mazoezi hayo yametajwa kuwa miongoni mwa makubwa zaidi kuwahi kufanyika kusini mashariki mwa Iran. Taarifa zinasema kuwa mazoezi hayo makubwa ya kijeshi yalifanyika kwa mafanikio na yalijumuisha makombora, mizinga, ndege zisizo na rubani, helikopta, magari ya deraya na vikosi maalumu vya makomando.

Wanajeshi walioshiriki katika luteka hiyo pia walifanya majaribio ya vita vya kielektroniki huku wakizingatia zaidi kuimarisha uwezo wa kumhujumu adui na kujihami.

Mwezi jana IRGC ilifanya mazoezi makubwa baharini katika pwani ya kusini mwa Iran katika Ghuba ya Uajemi na Lango Bahari la Hormoz.

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Meja Jenerali Hossein Salami amesema mazoezi hayo yana ujumbe wa wazi kwa utawala wa Kizayuni wa Israel. Aliongeza kuwa, ujumbe wa mazoezi hayo ni mzito kwa utawala wa Kizayuni kwamba unapaswa kuchukua tahadhari usifanye kosa lolote kwani ukiibua chokochoko basi mikono yake itakatwa.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amesema mbali na kuwa mazoezi hayo yanaonesha azma imara na isiyoterereka ya kulinda ardhi ya Kiislamu na kutoa jibu kali kwa maadui wa nchi hii, pia  yana ujumbe wa udugu na usalama kwa nchi rafiki na jirani.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*