?>

Jeshi la Iran la IRGC lashambulia ngome za magaidi Kurdistan, Iraq

Jeshi la Iran la IRGC lashambulia ngome za magaidi Kurdistan, Iraq

Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limelenga na kuharibu ngome za magaidi waliokuwa katika eneo lenye mamlaka ya ndani la Kurdistan, kaskazini mwa Iraq.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa taarifa ya tovuti ya Sepah News, Kikosi cha Nchi Kavu cha IRGC kimetekeleza oparesheni hiyo mapema Jumatano asubuhi.

Makundi  ya kigaidi kwa miaka kadhaa sasa chini ya himaya ya Marekani na utawala wa Kizayuni yamekuwa yakijaribu kuiwekea Iran mashinikizo ya juu kabisa kwa hujuma za kigaidi katika maeneo ya mipakani.

Kituo cha Hamza Sayyid Shuhadaa AS cha Kikosi cha Nchi Kavu cha IRGC kimetoa taaifa na kutangaza kwamba, opareseheni hiyo imefuatia chokochoko za hivi karibuni za makundi ya kigaidi yanayofungamana na madola ya Kiistikbari ambayo yamekuwa yakijipenyeza ndani ya ardhi ya Iran kwa lengo la kutekeleza hujuma za kigaidi.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, katika oparesheni maalumu ya kiusalama, timu moja ya magadii waliokuwa na silaha waliingia katika mtego wa maafisa wa usalama wa Kikosi cha Nchi Kavu cha IRGC ambapo magaidi wote wa kundi hilo ambao walikuwa watano walikamatwa katika eneo la Baneh katika mkoa wa Kurdistan nchini Iran.

Magaidi hao walikiri jinai zao za kigaidi ambazo zilikuwa na malengo mabaya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kwa msingi huo ngome za magaidi hao ambazo zilikuwa katika eneo la Kurdistan la Iraq zimelengwa kwa makombora ya Kituo cha Hamzah Sayyid Shuhadaa cha Kikosi cha Nchi Kavu cha IRGC na kuharibiwa kabisa.

Tarehe 12 Machi mwaka huu pia, vituo viwili vya kijasusi vya Shirika la Ujasusi na Operesheni Maalumu la utawala wa Kizayuni wa Israel (Mossad) mjini Erbil, mji mkuu wa eneo lenye mamlaka ya kujitawala la Kurdistan Kaskazini mwa Iraq, vilipigwa kwa makombora yaliyorushwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran.

Katika taarifa kufuatia oparesheni hiyo, IRGC ilisema "Usalama na amani ya ardhi ya Kiislamu ni mstari mwekundu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ,na hakuna upande wowote atakaoruhusiwa kuitishia au kuishambulia."342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*