?>

Jihadul-Islami: Tutawapindua majenerali wa Israel kwa mashambulio ya muqawama

Jihadul-Islami: Tutawapindua majenerali wa Israel kwa mashambulio ya muqawama

Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina imesema, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel unalitumia suala la kuanzisha uhusiano wa kawaida na nchi za Kiarabu kutekeleza sera yake ya kuiyahudisha Quds na kufuta malengo matukufu ya Palestina.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Msemaji wa harakati hiyo ya muqawama ya Palestina, Tariq Silmi amebainisha kuwa, utawala wa Kizayuni unapigania kupata ushindi katika mji wa Baitul Muqaddas unaoukalia kwa mabavu na unafanya juu chini ili kuimarisha uwepo wa wazayuni katika mji huo na kushika hatamu za mlingano wa nguvu.

Silmi amefafanua kuwa Gaza imefanikiwa kumpindua Benjamin Netanyahu, waziri mkuu aliyetangulia wa utawala wa Kizayuni; na kwa mashambulio ya harakati ya muqawama, inao uwezo wa kuwapindua majenerali wengine wa utawala huo.

Kiongozi huyo wa Jihadul-Islami ameashiria njama za utawala wa Kizayuni za kuziangamiza nchi za Kiarabu na akasema, adui mzayuni ni legelege na kila aliyeanzisha uhusiano naye wa kawaida inapasa ajitathimini upya katika mahesabu yake.

Tariq Silmi amesisitiza kuwa makundi ya Palestina yanaendelea kutathmini matukio ya msikiti wa Al Aqsa na wala hayatawatazama macho tu wazayuni bali yatatoa jibu kwa uvamizi wao dhidi ya msikiti huo mtukufu.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*