?>

Jinai mpya ya Wazayuni! Wamuua shahidi mwandishi wa al Jazeera kwa damu baridi kabisa!

Jinai mpya ya Wazayuni! Wamuua shahidi mwandishi wa al Jazeera kwa damu baridi kabisa!

Wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamefanya jinai nyingine ya kumuua kikatili na kidhulma, kwa damu baridi kabisa na kutokea nyuma, mwandishi mashuhuri na nguli wa televisheni ya al Jazeera, Shirin Abu Akleh alipokuwa katikati ya kazi zake kwenye kambi ya Jenin.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hadi hivi sasa wanajeshi makatili wa Israel wameshaua mamia ya waandishi wa habari, kuwateka nyara na kuwajeruhi wengine wengi. Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari huko Palestina ilitangaza hivi karibuni kuwa, shabaha ya utawala wa Kizayuni ya kuwateka nyara, kuwajeruhi na kuwaua shahidi waandishi wa habari ni kujaribu kuzuia kufichuliwa jinai zao wanazowafanyia wananchi madhlumu wa Palestina.

Televisheni ya al Jazeera imetangaza kuwa, pamoja na kwamba Shirin Abu Akleh alikuwa amevaa kikoti cha waandishi wa habari na cha kuzuia kupenya risasi, lakini wanajeshi makatili wamepiga risasi kichwani kwa kutokea nyuma na kwa makusudi.

Shaatha Hanaysha, mwandishi ambaye alikuwa pamoja na Abu Akleh ameiambia televisheni ya al Jazeera kuwa, wanajeshi wa Israel walikusudia kabisa kuua. Waandishi hao walikuwa kwenye eneo la wazi, wala Wapalestina hawakuwa wanafyatua risasi. Hivyo hakukuwa na sababu kabisa kwa wanajeshi hao kufyatua risasi na tena kumlenga kichwani kabisa mwandishi huyo.

Amesema, sote tulikuwa tumevaa vikoti vya waandishi wa habari na vya kujikinga na risasi pamoja na kofia maalumu za maeneo kama hayo. Hata kwa mbali tulionekana kuwa ni waandishi wa habari. Wanajeshi wa Israel walikuweko mbele na nyuma yetu, na hakukuwa na sababu kabisa ya kutupiga risasi.


342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*