?>

Kamalvandi: Ushirikano wa Iran na wakala wa IAEA unaendelea

Kamalvandi: Ushirikano wa Iran na wakala wa IAEA unaendelea

Msemaji wa Shirka la Nishati ya Nyuklia la Iran amezungumzia juu ya kuendelea ushirikiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Akijibu madai yaliyotolewa katika vyombo vya habari kwa kumnukuu Rafael Grossi Mkurugenzi Mkuu wa IAEA  kwamba mada za urani zimepatikana katika maeneo ambayo hayajatangazwa na kwamba Iran haijawajibika katika miezi iliyopita, Behruz Kamavandi Msemaji wa Shirika la Nishati ya Nyuklia la Iran  ameongeza kuwa, mwakilishi wa Iran katika wakala wa IAEA anachunguza taarifa hizo za ajabu na ambazo hazikutarajiwa za Rafael Grossi.  

Msemaji wa Shirika la Nishati ya Nyuklia la Iran wakati huo huo amesisitiza kuwa kinachoonekana ni kuwa,  kuna upotoshaji kuhusu taarifa zilizoenezwa zikimhusisha Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) jambo ambalo lilishawahi kutokea huko nyuma. 

Kamalvandi ameongeza kuwa sambamba na taarifa ya pamoja iliyosainiwa kitambo nyuma kati ya Wakala wa IAEA na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran; ushirikiano kuhusu masuala ya pande mbili unafuatiliwa na haupasi kutathminiwa na IAEA katika mazingira ya sasa.  

Vyombo vya habari vya Magharibi hivi karibuni vilimnukuu Rafael Grossi Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) akibainisha juu ya miradi ya nyuklia ya siri na pia kwamba Iran haijawajibika kuhusu madai ya kugunduliwa mada za urani katika taasisi zake za nyuklia ambazo hazikutangazwa awali. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*