?>

Kamanda: Utawala wa Kizayuni hauna uwezo wa kukabiliana na Iran

Kamanda: Utawala wa Kizayuni hauna uwezo wa kukabiliana na Iran

Kaimu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema utawala wa Kizayuni wa Israel hauna uwezo wa kukabiliana na Iran.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Brigedia Jenerali Mohammad Hussein Dadras Kaimu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo Jumatano katika mahafali ya kuhitimu wanajeshi na kuongeza kuwa: "Sababu ya utawala wa Kizayuni kupiga makelele ya ufokaji ni kutokuwa na ubavu wa kukabiliana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran; na iwapo itatokezea ukapatwa na hasira za Iran hautaweza kuinuka tena."

Kaimu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameendelea kusema kuwa, madola makubwa duniani yameamua kufanya mazungumzo na Iran kwa sababu ya nguvu za Jamhuri ya Kiislamu ambazo chimbuko lake ni baraka zitokanazo na maelewano ya kitaifa na Kiongozi Muadhamu mwenye busara."

Brigedia Jenerali Dadras aidha ameashiria machafuko na ukosefu wa usalama wa miaka ya karibuni katika eneo na kusema pamoja na kuwepo ukosefu wa usalama katika nchi jirani, Iran inashuhudia usalama kamili.

Jana pia Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC Meja Jenerali Hossein Salami alisema kuwa, Wamarekani sasa wameelewa kwamba, kama wataendelea kung'ang'ania kubakia katika eneo la Asia Magharibi, basi wajiandae pia kupata hasara kubwa zaidi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*