?>

Kamanda wa Marekani akiri juu ya umakini wa makombora ya balistiki ya Iran

Kamanda wa Marekani akiri juu ya umakini wa makombora ya balistiki ya Iran

Kamanda wa vikosi vamizi vya Marekani magharibi mwa Asia (CENTICOM) amekiri kuhusu uwezo na umakini wa makombora ya balistiki ya Iran.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Jenerali Kenneth McKenzie amesema alipohojiwa na jarida la Times kwamba makombora ya Iran yana uwezo wa kushambulia na kulenga shabaha kwa umakini mkubwa. Jenerali McKenzie amesema kuwa, kazi waliyofanya Wairani katika kipindi cha miaka mitatu hadi mitano iliyopita ni kuunda mfumo mkubwa wa makombora ya balistiki. 

Katika sehemu nyingine ya mahojiano hayo, kamanda huyo wa Marekani amekariri madai yake kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran na kueleza kuwa Rais wa Marekani amesema kuwa Iran haitamiliki silaha za nyuklia.  

Jenerali Kenneth McKenzie amebainisha hayo huku duru mpya ya mazungumzo kati ya Iran na kundi la 4 +1 linaloundwa na Ujerumani, China, Ufaransa, Uingereza na Russia ikitarajiwa kuanza tarehe 29 mwezi huu huko Vienna mji mkuu wa Austria.   

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeeleza wazi kuwa kipaumbele cha dharura na cha kwanza cha Tehran katika duru ya saba ya mazungumzo huko Vienna ni kuondolewa vikwazo vya kidhalimu na kinyume cha sheria vya Marekani dhidi ya Iran. 342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*