?>

Kanali Goïta asema Mali iko tayari kwa ajili ya mazungumzo na ECOWAS

Kanali Goïta asema Mali iko tayari kwa ajili ya mazungumzo na ECOWAS

Mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Mali, Assimi Goïta, amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) baada ya jumuiya hiyo kuiwekea vikwazo vikali nchi yake kutokana na serikali ya mpito kushindwa kuitisha uchaguzi mwezi ujao wa Februari mwaka huu kama ilivyopangwa hapo awali.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika hotuba yake kwa taifa, Kanali Assimi Goïta amesema ingawa amesikitishwa na maamuzi yasiyo ya kisheria wala ya kibinadamu yaliyochukuliwa lakini Mali iko tayari kwa ajili ya mazungumzo na ECOWAS kwa ajili ya kufikia mapatano yenye faida na maslahi kwa taifa la Mali na yanayoheshimu misingi mikuu ya jumuiya hiyo.

Goïta ametoa wito kwa wananchi wa Mali kuwa watulivu na akasema, "Tulichagua kuwa waaminifu ili kuamua hatima yetu kwa mikononi yetu kwa kutengeneza njia yetu wenyewe."

Nchi kadhaa za Magharibi mwa Afrika zimefunga mipaka yao ya nchi kavu na anga na Mali, na mashirika ya ndege ya nchi hizo pamoja na Ufaransa, yamefuta safari zao za kwenda Mali.

Haya yanajiri baada ya kundi la ECOWAS siku ya Jumapili, kuweka msururu wa vikwazo dhidi ya Mali, kutokana na serikali ya mpito kuakhirisha uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi ujao wa Februari. Serikali ya muda ya Mali imeakhirisha uchaguzi huo hadi Disemba mwaka 2025.

Nchi wanachama wa ECOWAS zimeamua kusimamisha biashara na Mali isipokuwa bidhaa za kimsingi, kukata misaada ya kifedha, na kufunga akaunti ya Mali katika Benki Kuu ya Mataifa ya Afrika Magharibi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*