?>

Katibu Mkuu wa UN akosoa ubaguzi katika ugavi wa chanjo ya corona

Katibu Mkuu wa UN akosoa ubaguzi katika ugavi wa chanjo ya corona

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa kushadidi kwa maambukizi ya virusi vya corona kunazidisha ukosefu wa usalama duniani na amekosoa ubaguzi unaoonekana katik ugavi usio wa kiadilifu wa chanjo ya corona.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Antonio Guterres ambaye jana alikuwa akihutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichojadili maudhui ya chanjo ya corona, amesema kuwa, ugavi wa chanjo hiyo unafanyika bila ya kuzingatia usawa na uadilifu.

Guterres ameashiria kwamba asilimia 75 ya chanjo ya corona iliyotolewa hadi sasa duniani imetolewa katika nchi 10 tu na amekosoa kuona kwamba nchi nyingine 130 hazijapata hata dozi moja ya chanjo hiyo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana Jumatano lilikutana kujadili ugavi wa chanjo ya corona duniani na jinsi ya kupambana na maambukizi ya Covid-19.

Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na kupeleka chanjo ya corona katika nchi zinazoendelea na jinsi ya kuwapa chanjo hiyo askari wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Takwimu za mtandao wa worldometers.info/coronavirus zinaonyesha kuwa, hadi sasa 110,435,805 wamepatwa na virusi vya corona kote duniani na 2,441,044 miongoni mwao wameaga dunia kutokana na virusi hivyo. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni