?>

Katibu Mkuu wa UN: Dunia inakabiliwa na kitisho cha Vita vipya Baridi

Katibu Mkuu wa UN: Dunia inakabiliwa na kitisho cha Vita vipya Baridi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametahadharisha kuwa, dunia hivi sasa inakabiliwa na kitisho cha Vita vipya Baridi vinavyoambatana na uchukuaji hatua za kinyuklia pamoja na changamoto zingine mbalimbali.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Guterres ameyasema hayo alipohutubia katika Chuo Kikuu cha Stone Hall jimboni New Jersey, Marekani na akabainisha kuwa, mbali na dunia kuanadamwa na kitisho cha Vita vipya Baridi vinavyoambatana na uchukuaji hatua za kinyuklia inakabiliwa pia na hatari ya ugaidi, wimbi la misimamo ya kufurutu mpaka na mapigano ya kikabila katika nchi zenye manung'uniko ya muda mrefu, ambapo kila moja kati ya changamoto hizo ni ishara kuwa dunia imekumbwa na mpasuko mkubwa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameendelea kueleza kwamba, mabadiliko ya tabianchi, ongezeko la tofauti za kimatabaka katika jamii mbalimbali na kushamiri  kwa baa la njaa na maradhi ni changamoto zingine ambazo dunia inakabiliana nazo.

Guterres amebainisha kuwa, dunia imeelemewa na mzigo mkubwa wa mizozo na migogoro ambayo imeshuhudiwa katika miongo iliyopita.

Katika hotuba yake hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amegusia pia vita vya Ukraine na kueleza kuwa, vita hivyo vimesababisha mateso kwa watu wengi, vifo na masaibu mengineyo.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*