?>

Katibu Mkuu wa UN Guterres alaani hujuma ya kigaidi Afghanistan

Katibu Mkuu wa UN Guterres alaani hujuma ya kigaidi Afghanistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amelaani vikali hujuma ya kigaidi katika eneo la Puli-e-Alam, jimbo la Logar nchini Afghanistan.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Duru za habari zinasema hujuma hiyo iliyotekelezwa na gaidi aliyekuwa akiendesha gari ililosheheni mabomu, imeua watu karibu 30.

Watu wengine wengi walijeruhiwa katika hujuma hiyo ya Ijumaa ambayo pia imeharibu makazi ya raia na miundombinu ikiwemo hospitali.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake mjini New York Marekani, Katibu Mkuu wa UN ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha, serikali na watu wa Afghanistan.

Amesema anatumai kwamba, mfungo wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ambao ni wakati wa kutafakari na kuonesha fadhila utakuwa wakati wa kuwakumbuka wale walioathirika na vita vya muda mrefu nchini humo na kushikamana katika juhudi mpya za kuelekea kwenye amani.

Mshauri wa Usalama wa Taifa nchini Afghanistan Hamdullah Mohib amelaumu kundi la Taliban kuwa limehusika katika hujuma hiyo mkoani Logar.

Wakati huo huo, wanamgambo wa Taliban wameituhumu Marekani kuwa imekiuka mapatano ya amani ya Doha kuhusu kuondoa askari wao vamizi nchini Afghanistan.

Kwa mujibu wa mapatano baina ya Taliban na Marekani, wanajeshi wote wa kigeni walipaswa kuondoka Afghanistan hadi kufikia jana Mei Mosi. Hata hivyo Rais Joe Biden wa Marekani amesema askari hao wataondoka Afghanistan ifikapo Septemba 11, 2021 wakati wa kutumia mwaka wa 20 tokea yafanyika mashambulio ya  kigaidi ya Septemba 11, 2002.

Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahed amesema kundi hilo litaamua ni hatua gani litakayochukua dhidi ya Marekani.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*