?>

Kenya yachukua hatua kali kuzuia maambukizi ya Ebola kuvuka mipaka ya nchi

Kenya yachukua hatua kali kuzuia maambukizi ya Ebola kuvuka mipaka ya nchi

Mamlaka za Afya ya Kenya zimetangaza kuwa, baada ya ugonjwa wa Ebola kuripotiwa tena nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hivi sasa Kenya iko katika kiwango cha juu cha tahadhari.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Dokta Samoel Khamadi, Mkurugenzi wa Kituo cha utafiti wa virusi katika Taasisi ya Matibabu ya Kenya (KEMRI) ameziambia duru za habari kwamba, vituo vyote vya kuingia nchini humo vimejiandaa kufanya upimaji wa virusi vya Ebola, huku idara za Afya zikifuatilia kwa makini shughuli za kuvuka mipaka ya nchi, hasusan kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Tahadhari hiyo ya Kenya inakuja siku chache baada ya kuripotiwa kesi mpya za ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hivi karibuni wasiwasi uliibuka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya mtu wa pili kuripotiwa kufariki dunia kwa maradhi hatari ya Ebola.

Wataalamu wanasema kuwa, maambukizi ya sasa yanaaminika kutoka kwa mnyama na wala sio kutokana na maambukizi ya awali kati ya binadamu.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, mwaka jana 2021 serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilitangaza kuwa, mlipuko mpya wa homa ya Ebola uliozuka kwenye jimbo la Kivu ya Kaskazini mnamo mwezi Oktoba ukiwa ni wa pili kwa mwaka huo umemalizika.

Ikumbukwe kuwa, mlipuko mkubwa zaidi wa ugonjwa hatari wa Ebola ulitokea baina ya Disemba 2013 na Aprili 2016 na kuua zaidi ya watu 11,000 katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone huko magharibi mwa bara la Afrika.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*