?>

Khatibzadeh: Ili kuhuisha JCPOA, ni dharura Marekani kuondoa kivitendo vikwazo dhidi ya Iran

Khatibzadeh: Ili kuhuisha JCPOA, ni dharura Marekani kuondoa kivitendo vikwazo dhidi ya Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema njia pekee ya kuhuisha mapatano ya nyuklia ya JCPOA ni Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya Iran.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Saeed Khatibzadeh, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameyasema hayo katika ujumbe wa Twitter alioutuma siku ya Ijumaa baada ya Mwakilishi wa muda wa Marekani katika Umoja wa Mataifa kumwandikia barua Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la umoja huo na kuondoa madai ya serikali iliyotangulia ya nchi hiyo kuhusu kurejeshwa vikwazo vyote vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran. Khatibazadeh ameongeza kuwa, baada ya Marekani kujiondoa katika mapatano ya JCPOA, hivi sasa kundi hilo linajumuisha tu Iran na nchi za kundi la 4+1 na wala si 5+1 wakati mapatano hayo yalipofikiwa.

Katika ujumbe wake wa Twitter, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekumbusha kuwa Donald Trump ndiye aliyeiondoa Marekani katika mapatano ya JCPOA na hivyo kuyavuruga kabisa. Kwa msingi huo, amesisitiza kuwa, ili kuhuisha tena kundi la 5+1 Marekani inapaswa kuondoa vikwazo dhidi ya Iran kivitendo.

Serikali ya zamani ya Marekani chini ya uongozi wa Rais Donald Trump mwezi Agosti mwaka jana baada ya kushindwa kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Iran ilianzisha harakati zilizofeli kwa ajili ya kuirejeshea Iran vikwazo vya Umoja wa Mataifa. 

 Kurudi nyuma huko kwa Marekani kunajiri katika hali ambayo serikali mpya ya sasa ya nchi hiyo chini ya uongozi wa Rais Joe Biden imekiri kufeli sera za mashinikizo ya juu kabisaTrump mkabala na Iran na kueleza kuwa ina lengo la kurejea katika mapatano ya JCPOA yaliyopasishwa na Baraza la Usalama kwa kuzingatia kujitoa Marekani kwa upande mmoja ndani ya mapatano hayo; hatua iliyopelekea kutengwa Marekani kimataifa. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni