?>

Khatibzadeh: Msimamo wa Iran katika mazungumzo ya Vienna ni kuondolewa vikwazo vyote

Khatibzadeh: Msimamo wa Iran katika mazungumzo ya Vienna ni kuondolewa vikwazo vyote

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, msimamo thabiti wa Tehran katika mazungumzo na kundi la 4+1 ni kuondolewa kikamilifu vikwazo vyote vya Marekani dhidi ya taifa hili.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Saeed Khatibzadeh amesema hayo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo amebainisha kwamba, msimamo na siasa thabiti za Iranh ni kurejea kikamilifu Marekani katika utekelezaji wa ahadi zake kwa mujibu wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tena neno kwa neno.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Iran haina haraka na wala haitangia katika mchezo mchafu na kwamba, kurejea huko kwa Marekani kunapaswa kuwe ni kwa mkupuo, urejeaji wenye uthabiti na ambao itawezekana kuufanyia tathmini.

Aidha amesema kuwa, safari ya hivi karibuni ya Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran katika eneo la Ghuba ya Uajemi haikuwa na uhusiano wowote na mazungumzo ya Kamisheni ya Pamoja ya JCPOA huko Vienna Austria.

Kuhusiana na kuenea habari ya kubadilishana wafungwa baina ya Iran na Marekani, Khatibzadeh amesema, suala la wafungwa ni kadhia ya kibinadamu na imekuwa ikifuatiliwa kando na mazungumzo mengine yanayohusiana na mazungumzo ya nyuklia ya JCPOA au masuala yanayohusiana na kadhia  hiyo.

Khatibzadeh ameashiria pia suala la mazungumzo ya Iran na Saudia na kuchukuliwa hatua za kuanzishwa uhusiano rasmi na kusema wazi kuwa, Iran daima imekuwa iko tayari kufanya mazungumzo kwa namna yoyote na katika ngazi yoyote na majirani ikiwemo Saudi Arabia.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*