?>

Khatibzadeh: Ripoti ya UN dhidi ya Iran ni ya kisiasa na haina insafu

Khatibzadeh: Ripoti ya UN dhidi ya Iran ni ya kisiasa na haina insafu

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Saeed Khatibzadeh amesema, azimio lililopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Iran limetokana na matashi ya kisiasa, la kiuhasama na halikuzingatia insafu.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Kwa kutegemea madai kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Iran, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewasilisha ripoti inayozungumzia masuala mbalimbali yakiwemo madai ya ukiukaji haki za binadamu nchini Iran na kukosoa utekelezaji wa sheria za haki za binadamu hapa nchini. Aidha ameitaka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itoe mashirikiano kwa ripota maalumu wa haki za binadamu wa umoja huo.

Akijibu suali la mwandishi wa habari wa shirika rasmi la habari la Iran IRNA kuhusu azimio la karibuni la Baraza Kuu la UN na ripoti ya muda ya Katibu Mkuu wa umoja huo kuhusu hali ya haki za binadamu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Khatibzadeh amesema, "kama ilivyokwisha sisitizwa mara kadhaa, maazimio kama haya yanatokana na matashi ya kisiasa, ni ya kiuhasama na yasiyozingatia insafu, na hayaandaliwi kwa muelekeo wa kustawisha haki za binadamu, ambalo ni miongoni mwa majukumu makuu ya taasisi za kimataifa za haki za binadamu; zaidi ni kwamba huwa hayakubaliwi kwa kauli moja na nchi wanachama".

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran ameongezea kwa kusema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepeleka kwa ofisi ya Katibu Mkuu wa UN maoni na hoja fafanuzi na zenye ushahidi kwa kila kipengele cha madai ya Guterres, lakini kwa masikitiko zimepuuzwa kwa namna maalumu.

Saeed Khatibzadeh amesisitiza kwa kusema: inasikitisha kuona ripoti iliyotolewa kwa kutumia jina la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa imetegemea madai yasiyo sahihi na nyaraka na ushahidi usio na itibari; na ndio maana sehemu kubwa ya matini ya asili ya ripoti hiyo imeratibiwa kulingana na vifungu vya madai na tuhuma za makundi yenye uadui na Iran na matapo ya kigaidi, lakini majibu ya ufafanuzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ripoti hiyo zitapatiwa nchi zote katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran ameonyesha kushangazwa pia na kutobainishwa ndani ya ripoti hiyo masuulia na dhima wanayobeba wawekaji na watekelezaji wa vikwazo dhidi ya Iran wala kutolewa ufafanuzi kuhusua athari hasi, haribifu na zenye kudhuru na kuua za hatua za mabavu za upande mmoja ambazo zinapingana na sheria, za kidhalimu, za kijinai na za ukiukaji haki za binadamu za taifa la Iran zilizochukuliwa na Marekani na dhima inayobeba nchi hiyo kimataifa juu ya suala hilo.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*