?>

Khatibzadeh: Utawala wa Kizayuni wa Israel unaogopa kutangazwa habari sahihi na za kweli

Khatibzadeh: Utawala wa Kizayuni wa Israel unaogopa kutangazwa habari sahihi na za kweli

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali jinai ya utawala haramu wa Israel ya kumuua kwa kupiga risasi Shirin Nasri Abu Aqleh mwandishi habari Mpalestina wa Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Saeed Khatibzadeh amesema kuwa, utawala ghasibu wa Israel una hofu na woga wa kutangazwa habari sahihi na za kweli.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kutoa mkono wa pole kwa familia ya shahidi huyo na taifa la Palestina amesema kuwa, hatua hii ya kijinai ya Israel ni ushahidi wa wazi kwamba, utawala huo ghasibu hauheshimu kabisa tasnia ya habari.

Aidha amesema kuwa, kinyume kabisa na madai na propaganda zake, utawala haramu wa israel una woga na wahaka mkubwa wa kutangazwa habar sahihi na ndio maana umefikia hatua ya kumuua kwa kumpiga risasi mwandishi wa habari aliyekuwa katika majukumu yake ya upashaji habari.

Shirin Nasri Abu Aqleh mwandishi mkongwe wa habari Mpalestina wa Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar aliuawa shahidi kwa kupigwa risasi jana na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel alipokuwa akiakisi machafuko katika kambi ya wakimbizi Wapalestina mjini Jenin.

Vikosi vya Israel vimewakamata, kuwajeruhi au kuwauwa shahidi mamia ya waandishi wa habari hadi sasa. Hivi karibuni Kamati ya Kuwalinda Waandishi wa Habari wa Palestina ilieleza kuwa, hatua za kiuadui za utawala wa Kizayuni dhidi ya waandishi wa habari zinalenga kuficha jinai za utawala huo ghasibu dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*