?>

Ujumbe wa kiongozi wa Iran katika msimu wa Hija/ tunapinga vitendo vya ubaguzi Marekani na tunaunga mkono harakati za wananchi nchini humo

Ujumbe wa kiongozi wa Iran katika msimu wa Hija/ tunapinga vitendo vya ubaguzi Marekani na tunaunga mkono harakati za wananchi nchini humo

Kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran amesema: vitendo vya Marekani kuyaelekea mataifa dhaifu, ni dalili tosha ya ubaguzi wa taifa hilo, pia kitendo cha Polisi cha kumkanyaga shingoni mwanachi asiokuwa na hatia ni katika mambo yanaonyesha kutokuwa na utu kwa utawala huo.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Ayatollah Sayyed Ali Khamenie ametoa ujumbe Kufuatia mnasaba wa msimu wa ibada ya Hija Kwa waislamu waislamu ulimwenguni, ambapo amesisitiza umoja na mshikamano baina ya waislamu na waiumini duniani katika kubaliana na ubeberu wa Marekani na utawala Haramu wa Israel, pia amesisitiza kuwasaidia wapelestina ambao wapo katika mazingira magumu ya vitendo vya dhulma alkadhalika kuwahurumia wananchi wasiokiwa na hatia nchini Yemen na waislamu wote wanaodhoofishwa ulimwengu, pia nawanasihi viongozi wa mataifa ya kiislamu kuacha uhusiano na Utawala Haramu wa Israel wakitafuta manufaa binafsi ya hapa duniani, Kwa upande mwingine ameashiria madhara ya uwepo wa Marekani katika eneo la Magharibi mwa mashiriki ya kati kwakusema:

Uwepo wa Marekani magharibi mwa Asia, kunaleta maafa makubwa kwa wakazi wa eneo hilo ambapo kuna sababisha kuondoka kwa amani na usalama, uharibifu, na kuchelewesha maendeleo ya mataifa hayo, kwa upande mwingine kuhusu matukio yanayojiri hivi sasa nchini Marekani ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo, Kwa asilimia zote tunaungana na wananchi na kupinga hatua za kikatili zinazochukuliwa dhidi ya wananchi wanaoandamana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo.

ujumbe kamili wa kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiisalamu ya Iran kwa mnasaba wa msimu wa Hija ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Namshukuru mwenyezi Mungu mlezi wa walimwengu, kisha sala na salamu zimuende Muhammad na kizazi chake kitwagarifu na maswahaba wake walio wema na wale waliowafuata Kwa wema mpaka siku ya malipo.

Msimu wa Hajj, ambao kila wakati ulikuwa msimu wa kupata nguvu na ustawi wa ulimwengu wa Kiisilamu, mwaka huu nyoyo za waumini zimekuwa na huzuni na hisia za kujitenga na kutofaulu kwa wale waliotamani kutekeleza ibada hii ndani ya mwaka huu. Mioyo huwa na simanzi kutokana na kushindwa kuifikia Kaaba katika ibada ya Hija, na kauli ya Labaika na kuitikia wito wa Allah kwa wale waliokuwa na matarajio ya kutekeleza ibada hiyo wamebaki na majonzi na na machuzi kuwatoka.

Bila shaka kushindwa kutkeleza kwa ibada hii ni kwa muda mfupi na hautadumu na hali hii kwa uwezo wa Mungu, lakini somo la kuthamini baraka kubwa ya Hajj lazima litunzwe na kutuweka huru mbali na kupuuzwa.Siri ya ukuu na nguvu ya Umma wa Wakiislam katika kundi linalozunguka na la Waumini wengi katika sehemu takatifu ya Kaaba na haramu ya bwana Mtume (s.a.w.w) na Maimamu wa Baqii (as) lazima tuhisi huzuni na kutafakari kuhusu suala hili kwa mwaka huu.

Hajj ni wajibu usio na kifani; ambao unanafasi kubwa katika mambo ya wajibu katika uislamuni kana kwamba mambo yote muhimu ya kibinafsi na ya kijamii, ya kidunia na akhera, kiroho na kimada na kihistoria ya ulimwengu, tunapaswa kutafakari na kujifunza katika suala zima ibada hii tukufu.

Ndani yake kuna mafuzno ya kiroho lakini bila ya kujetenga na jamii, ndani yake kuna mambo ya kijamii bila vurugu na migogoro na kejeli na kuwakandamiza wengine. Kwa upande mwengine katika Hijja kuna fungamano la kiroho na mwenyezi Mungu kwa maombi na ibada mbalimbali na kwa upande mwingine kuna fungamano na unganisho la umoja na mawasiliano watu.

Haji anaangalia kwa jicho moja katika uhusiano wake wa muda mrefu na historia ya Ibrahim, Ishmael na Hajar, na Mjumbe wa Mungu Muhammad alipoingia kwa ushindi katika Msikiti Mtakatifu wa Makka pamoja na umati wa waumini wa karne ya kwanza, kwa upande mwingine akiangalia idadi kubwa ya waumini wa zama zake wanaoingia katoika sehemu hiyo takatifu, jambo ambalo linaweza kutuweka pamoja tukashikamana na kamba ya mwenyezi Mungu na umoja wa kiislamu hatimaye kusonga mbele kwa pamoja.

Kutafakari juu ya hali ya Hija kunamfanya anaekwenda kuhiji kuamini kwa dhati kwamba maoni na matarajio ya dini kwa wanadamu hayatatimizwa bila huruma na ushirikiano wa kikundi cha watu wa dini moja, na kwa kupatikana kwa huruma hii na ushirikiano huu, vitimbi vya maadui na wapinga haki hivitakuwa na madhara yeyote kwa waumini walioshikamana katika kamba ya Mungu.

Hija ni maonyesho ya nguvu dhidi ya wanaojivuna na mabeberu ambao ni kitovu cha ufisadi, ukandamizaji, mauaji ya watu wasiokuwa na nguvu, mauaji na uporaji, ambapo hivi sasa mwili na roho ya Umma wa Kiislam umekuwa na huzuni na majonzi kutokana na mateso na kumwagika damu zao kwa kukandamizwa. Hivyo basi Hija ni maonyesho ya uwezo mkubwa ambapo kwa upande mmoja ni nguvu nzito na laini dhidi ya maadui wake.

Hii ndio asili ya Hija kiroho na sehemu muhimu zaidi ya malengo ya Hija, na kwa sababu hiyo ndio maana Imam Khomeini aliita kuwa ni Hija ya Ibrahim, na hii ndio maana tunasema kwamba kama wanaosimamia sula la Hija ambao wanajiita watumishi wa Hramu za mwenyezi Mungu, kama watatekeleza nyadhifa zao kwa dhati, kwa maana watafute radhi za Mungu badala ya kutafuta kuwaridhisha Marekani, ambapo kwakufanya hivyo itakuwa ni sababu ya kutatua shida na matatizo mengi ya ulimwengu wa Kiislamu.

Leo, kama siku zote - na zaidi ya hapo zamani – maslahi ya uma wa kiislamu yapo katik umoja wao;Umoja ambao watashikamana kwa mkono mmoja dhidi ya vitisho na uadui wa Shetani mkubwa ambaye ni Marekani, Marekani iliokuwa na vitembi mbalimbali, na kuhujumu mataifa mengine wakishirikiana na utawala haramu wa kizayuni.

Hii ndio maana ya amri ya Mungu aliposema:“وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا” shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane.

Qur`an hakim imeutangaza uma wa kiislam kuwa “أَشِدَّاءُ عَلَی الْکُفَّارِ رُحَمَاءُ بَیْنَهُمْ  “ni wakali kwa makafiri na uhurumiana baina yao.Huku ikiamuru kuwa " وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا "Wala msiwategemee wanao dhulumu," وَلَن يَجْعَلَ اللَّـهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلً"wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini, “فَقَاتِلُوا أَئِمَّةَ الْکُفْرِbasi piganeni na viongozi wa ukafiri, “لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَMsiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki. Na kuwata kuwa na tahadhari na maadui zao, na baada ya kuwajua maadui zao mungu anatutaka hivi “لا یَنْهَاکُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِینَ لَمْ یُقَاتِلُوکُمْ فِی الدِّینِ وَلَمْ یُخْرِجُوکُم مِّن دِیَارِکُمْ” Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu.

Amri hizi muhimu hazipaswi kutengwa kamwe katika mfumo wetu wa kifikra na mambo yenye thamani kwetu Waislamu na hazipaswi kusahaulika semi hizo.

Leo, zaidi siku zote, msingi wa mabadiliko unapatikana kwa umma wa Kiislamu na wataalamu na wanafikra wa uma huu. Leo hii mwamko wa Kiislamu kwa maana ya kurejea kwa wataalamu na vijana wa kiislamu kuzingatia athari za kielimu na maarifra ya kiislamu, ni jambo ukweli na uhakika usiofichika.Leo, Ukomunisti ambao una miaka mia toka uanze na kushika nafasi yake kwa miaka hamsini, ambayo imetengeza tamaduni mzima wa mataifa ya Ulaya, leo hii utamaduni huo umeporoma kwa ghafla na kuonekana aibu na matatizo ya mfumo huo, na kusababisha mtafaruku marumbano katika ulimwengu wa sasa.

Leo, sio tu upande wa kitamaduni wa Magharibi - ambayo umepata aibu na kashfa tangu mwanzo - bali hata upande wa kisiasa na kiuchumi, ambao umesimamia demokrasia na misingi ya kipato na ubepari na ubaguzi, imeonyesha kutokuwa na tija na umekuwa na ufisadi mkubwa wa kijamii.

Leo, kuna wasomi wengi katika ulimwengu wa Kiislam ambao, wameimua shingo kwa fahara, wanasema kuwa utamaduni wa kimagharibi hauna tija huku wakionyesha kwa wazi njia mbadala za Kiislamu zinazoenda kinyume na mitazamo ya kimagaharibi.Bali hata wanafikira wa Magharibi, ambao hapo awali walijigamba kutangaza mitazamo ya kimagharibi kuwa kama mwisho wa historia, sasa wanakubali mitazamo ya Kiislamu ambayo inaweza kutatua changamato za ukandamizaji ziliopo hivi sasa duniani.

Jaribuni Kuangalia mitaa ya Marekani, kunako maamuzi ya viongozi wao wanavyowafanyia wananchi wao, ambapo wamefika katika kina kerefu cha umbali wa mataba nchini humo, unyonge na ujinga wa wale waliochaguliwa kuendesha nchi hiyo, ubaguzi wa rangi mbaya katika nchi hiyo.Ukatili wa afisa ambaye humuuwa mtu ambaye hana hatia mbele za watu barabarani, pia matatizo ya kimaadili kijamii katika tamaduni ya kimagharibi na upotovu wa falsafa ya siasa na uchumi wa mataifa hayo ni ishara tosha ya kushindwa kwa nadhariua hizo.

Mienendo ya wamarekani kwa mataifa dhaifu ni vielelezo tosha kwa walimwengu, kitendo alichokifanya yule Polisi aliomkandamiza kwa kote lake katika shingo ya mtu mweusi asiyekuwa na utetezi hata akafariki ni katika vielelezo hivyo.

Serikali zingine za kimagharibi kila moja, kwa kiwango chake kinachowezekana, ni katika mifano inayoweza kutolewa katika janga hili.

Hija ya Ibrahim ni jambo tukufu la Uislam katika kukabiliana na ujahili na ujinga huu wa kisasa; kulingania katika Uisilamu na kuonyesha mfano wa maisha ya kijamii ya Kiisilamu, Jamii ambayo umoja wa waumini, katika harakati zinazozunguka mhimili wa Tawhid, ni ishara kubwa ya kuepuka migogoro, Kuepuka ubaguzi na upendeleo wa kidemokrasia, kuepuka rushwa na uchafuzi wa mazingira, ni jambo la muhimu na lamsingi; kurusha mawe dhidi ya shetani na kujiweka mbali na washirikina na kujikurubisha na wanyonge na kuwasaidia masikini na kukuza alama ishara za watu wenye imani na waumini, ni kati ya majukumu makubwa tulionayo, ambapo hata kufikia masilahi ya umma na masilahi ya pamoja na kumkumbuka Mungu na kumshukuru na kumtumikia ndio malengo muhimu na yamsingi.

Hii ni taswira ya jumla katika uislamu kwa kumuiga Nabii Ibrahim, ukilinganisha na tamaduni za Kimagharibi, ambapo kupitia mioyo ya kila muislamu mwenye bidii na shauku ya kujitahidi, tutafanikisha kupata jamii makini.

Sisi, wananchi wa Irani, chini ya mwongozo na uongozi wa Imam Khomeini, tukiwa na shauku hiyo tumeshapiga hatua, Hatusemi kuwa tumeweza kufikia kila tunachokitaka na kupenda. Isipokuwa tunasema kwamba tumetoka mbali na kuondoa vizuizi vingi. Kwa baraka za kuamini ahadi iliotolewa katika Qur`an, hatua tuliopiga imekuwa thabiti, Shetani mkubwa zaidi na shetani mtapeli wa wakati huu, ambaye ni serikali ya Marekani, hajaweza kututisha au kusimamisha harakati yetu, au kusimamisha maendeleo yetu ya nyenzo na kiroho.

Tunaamini kuwa mataifa yote ya Kiislamu kuwa ni ndugu zetu, na tunawachukulia wasio Waislamu ambao hawajatuhujumu kuwafanyia uadilifu na kuwatendea haki.Tunazingatia kuwa huzuni na mateso ya jamii za Waislamu duniani ni mateso yetu na tunfanya juhudi kubwa ya kutatua matatizo hayo, tutaendelea kujitahidi kuwasaidia Wapalestina waliyokandamizwa, pia tunawahurumia wale walijeruhiwa nchini Yemen na kuwajali Waislamu waliokandamizwa kila mahali.

Ni jukumu letu kushauri viongozi wa nchi za Kiislamu; Maafisa wa serikali ambao, badala ya kumtegemea ndugu yao Mwislamu, hukimbilia mikononi mwa adui na huvumilia unyonge kwaajili ya faida chache ya dunia, na kuondoa heshima na uhuru wa taifa lao.Ama wale ambao wamekubali kubaki kwa utawala haramu wa Israel na kufanya juhudi za wazi na maficho kufanya kuweka uhusiano nao, tunasihi kuacha kufanya hivyo na tunawatahadharisha sasa na hilo.

Uwepo wa Marekani magharibi mwa Asia, kunaleta maafa makubwa kwa wakazi wa eneo hilo ambapo kuna sababisha kuondoka kwa amani na usalama, uharibifu, na kuchelewesha maendeleo ya mataifa hayo, kwa upande mwingine kuhusu matukio yanayojiri hivi sasa nchini Marekani ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo, Kwa asilimia zote tunaungana na wananchi na kupinga hatua za kikatili zinazochukuliwa dhidi ya wananchi wanaoandamana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo.

Mwisho, tunatoa salamu na baraka kwa imam Zaman, na kumkumbuka Imam Khomeini pia ninatuma salamu kwa roho za mashujaa na kumtakaMwenyezi Mungu Mtu azipe furaha roho zao, na kuwatakia Hija njema isiokuwa na hofu katika miaka ijayo, amin.

 

   Sayyed Ali Khamenei

   28/6/2020


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*