?>

Kiongozi Muadhamu amteua Mohseni-Ejei kuwa Mkuu mpya wa Vyombo vya Mahakama Iran

Kiongozi Muadhamu amteua Mohseni-Ejei kuwa Mkuu mpya wa Vyombo vya Mahakama Iran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemteua Gholamhossein Mohseni-Ejei kuwa Mkuu mpya wa Vyombo vya Mahakama vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika dikrii, Ayatullah Ali Khamenei amemtaka Mohseni-Ejei kutazama kwa makini dhamira na malengo ya Idara ya Mahakama kama yalivyoainishwa kwenye Katiba ya nchi, sambamba na kuendelea kufuata njia ya mageuzi.

Kiongozi Muadhamu amemuasa Mkuu mpya wa Vyombo vya Mahakama vya Iran kutumia teknolojia mpya kufanikisha shughuli za taasisi hiyo, na vile vile kuwateua shakhsia wachapakazi na waaminifu.

Kadhalika Ayatullahi Khamenei amemtaka Mohseni-Ejei kuendeleza kwa nguvu vita dhidi ya ufisadi mbali na kuwa na mtagusano na mawasiliano ya moja kwa moja na wananchi.

Gholamhossein Mohseni-Ejei ambaye alikuwa Naibu Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, anakuja kurithi mikoba ya Rais mteule wa Iran, Hujjatul Islam Walmuslimin Ebrahim Raeisi.

Sayyid Ebrahem Raeisi alitangazwa mshindi katika kinyang'anyiro cha urais cha Juni 18 mwaka huu, kwa kupata kura karibu milioni 18 za wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*