?>

Kiongozi Muadhamu: Endelezeni mapambano halali dhidi ya utawala ghasibu, ulazimike kukubali kura ya maoni

Kiongozi Muadhamu: Endelezeni mapambano halali dhidi ya utawala ghasibu, ulazimike kukubali kura ya maoni

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, harakati ya kuporomoka na kutoweka utawala wa Kizayuni imeanza na haitasimama; na akawahutubu Mujahidina wa Palestina kwa kuwaambia: "Endelezeni mapambano halali dhidi ya utawala ghasibu ulazimike kukubali kura ya maoni.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo leo katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds. Ayatullah Khamenei ameashiria mabadiliko makubwa ya mlingano wa nguvu yaliyotokea kwa manufaa ya Ulimwengu wa Kiislamu na kambi ya muqawama, mkabala na kufifia waziwazi nguvu za Marekani na utawala wa Kizayuni; na akasema, kuanzisha uhusiano wa kawaida na nchi chache dhaifu hakutazuia mwenendo wa kutoweka utawala ghasibu wa Kizayuni; na sambamba na kusisitiza kutekelezwa takwa la kimantiki la kuitishwa kura ya maoni kwa kushirikisha wakazi wote wa asili wa Palestina ili kuamua mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo, amewahutubu mujahidina wa Palestina akisema: Endelezeni mapambano yenu halali na ya kiakhlaqi dhidi ya utawala ghasibu mpaka uwe hauna budi kukubali takwa hilo endelevu.

Qatika hotuba yake hiyo aliyotoa kupitia vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia mantiki iliyo dhaifu kupindukia iliyotumiwa kuasisi utawala wa Kizayuni na akasema "kwa zinavyodai zenyewe, nchi za Ulaya ziliwadhulumu Mayahudi katika miaka ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, lakini zinasema, kisasi cha Mayahudi inapasa kilipizwe kwa kuwafanya wakimbizi watu wa taifa moja katika Asia Magharibi na kwa mauaji ya kinyama ndani ya nchi hiyo. Kwa kufanya hivyo, zimeyabatilisha madai yao ya uongo kuhusu haki za binadamu na demokrasia.

Amekumbushia pia ukweli kwamba "tokea siku ya mwanzo, Wazayuni waliigeuza Palestina kuwa kituo cha ugaidi" na akabainisha kuwa: "Israel si nchi, bali ni kambi ya kigaidi iliyo dhidi ya taifa la Palestina na mataifa mengine ya Waislamu; kwa hivyo kupambana nayo ni kupambana na dhulma na ugaidi na ni jukumu la watu wote.

Ayatullah Khamenei ameashiria matukio yaliyojiri kabla ya kuasisiwa utawala ghasibu, yaani "uingiliaji mkubwa wa Magharibi katika eneo na kuziweka madarakani tawala vibaraka na za kidikteta", na akasema, udhaifu na mfarakano wa ndani ya umma wa Kiislamu ndio ulioandaa mazingira ya kughusubiwa Palestina; na akaongezea kwa kusema: katika kipindi kile, kambi zote mbili za Ubepari na Ukomunisti ziliungana pamoja na maqaruni wa Kizayuni; Uingereza ikabuni njama yenyewe, mabepari wa Kizayuni wakasimamia utekelezaji wake kwa fedha na silaha, na Urusi ikapeleka huko umati mkubwa wa Mayahudi ikiwa nchi ya kwanza kuutambua rasmi utawala huo haramu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ametilia mkazo pia kuungana pamoja nchi za Kiislamu katika kadhia ya Palestina na kwa ajili ya hatima ya Quds tukufu na akasema: kuungana pamoja huko ni jinamizi kwa adui Mzayuni na waungaji mkono wake wa Marekani na Ulaya; na mpango uliofeli wa Muamala wa Karne na hatua ya nchi chache dhaifu za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu ni juhudi za kutapatapa za kujaribu kulikimbia jinamizi hilo.

Ayatullah Khamenei amesema "kuendelea muqawama ndani ya ardhi za Palestina na kuimarisha njia ya jihadi na kufa shahidi" na "uungaji mkono wa nchi za dunia na mataifa ya Waislamu kwa mujahidina wa Palestina" ni nukta mbili muhimu zitakazoamua hatima ya mustakabali; na akaongeza kwamba: harakati hii ya pande zote itabatilisha njama ya maadui; na kila mmoja, kuanzia viongozi, wanafikra, maulamaa, vyama, makundi na vijana anapaswa kuijua nafasi yake na kutoa mchango wake.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*