?>

Kiongozi Muadhamu: Kikosi cha Quds kizuizi kikubwa athirifu cha diplomasia legevu katika Asia Magharibi

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) ni sababu kubwa kabisa athirifu ya kuzuia diplomasia legevu na isiyo na irada katika eneo la Asia Magharibi.


Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amesema hayo leo katika hotuba yake kwa mnasaba wa Siku ya Wafanyakazi Duniani na Siku ya Mwalimu ambapo sambamba na kukosoa matamshi yanayotolewa na viongozi rasmi wa nchi ambayo yanatumiwa vibaya na maadui amesisitiza kwamba,  Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) ni sababu kubwa kabisa athirifu ya kuzuia diplomasia legevu na isiyo na irada katika eneo la Asia Magharibi.

Ayatullah Khamenei amekosoa faili la sauti ambalo liko mikononi mwa vyombo vya maadui na wapinzani wa Jamhuri ya Kiislamu na kueleza kwamba, kwa miaka mingi sasa Wamarekani wamekasirishwa na ushawishi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema pia katika hotuba yake hiyo kwamba, ni kwa sababu hiyo ndio maana Wamarekani hawakuwa wakimpenda shahidi Qassim Suleimani na ndio maana wakamuua shahidi.

Ayatulllah Khamenei ameongeza kuwa, hatupaswi kusema mambo ambayo yatakuwa na maana ya kama vile tunakariri matamshi ya maadui.

Kadhalika Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, madola ya Magharibi yamekuwa yaking'ang'ania na kutaka sera za kigeni za Jamhuri ya kiislamu ya Iran ziwe chini ya bendera yao, hili ndilo wanalotaka, kwa sababu kwa miaka mingi hali ilikuwa hivyo (kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu).

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*