?>

Kiongozi Muadhamu: Wafanyakazi wako mstari wa mbele kukabiliana na adui

Kiongozi Muadhamu: Wafanyakazi wako mstari wa mbele kukabiliana na adui

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema wafanyakazi ni nguzo kuu katika hema la uzalishaji bidhaa na kuongeza kuwa: "Wafanykazi wako katika mstari wa mbele kukabiliana na adui."

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo leo mjini Tehran wakati alipoonana na wafanyakazi na kusema lengo la mkutano huo ni kushukuru na kutambua jitihada za wafanykazi. Katika kikao hicho, amesisitiza kuhusu thamani ya kazi na kuashiria kuhusu mtazamo wa Uislamu kwa 'mfanyakazi' na 'kazi' na kusema: "Kinyume na mtazamo wa unyanyasaji wa mfumo wa kibepari na mtazamo wa kinara wa mfumo uliosambaratika wa kikomunisti, mtazamo wa Uislamu kwa mfanyakazi ni mtazamo wa kumshukuru na kutambua thamani yake na ni kwa msingi huu ndio Mtume Mtukufu wa Uislamu SAW alikuwa akiibusu mikono ya wafanyakazi."

Ayatullah Khamenei amesema wafanyakazi nchini Iran wameweza kupata mafanikio makubwa katika nyuga za kijeshi, kiuchumi na kisiasa na mfano wa hilo ni wafanyakazi wasiopungua 14,000 ambao walitoa maisha yao mhanga katika vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran katika muongo wa 80.

Akiashiria mafanikio ya wafanyakazi katika uga wa kiuchumi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema moja ya sera za madola ya kiistikbari tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ilikuwa ni kuvuruga uzalishaji wa kiviwanda nchini Iran na katika miaka ya hivi karibuni hilo limejidhihirisha katika vikwazo lakini wafanyakazi kwa kusimama kidete wamezuia maadui kufikia lengo hilo na hivyo katika uga huu wamekuwa ni nguzo asili ya uzalishaji. 

Ayatullah Khamenei pia ameashiria namna wafanykazi wamekuwa wakichochewa tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema, lengo la uchochezi huo ni kubadilisha jamii ya wafanyakazi kuwa nembo ya malalamiko lakini hapa pia katika uga wa kisiasa, waliokuwa wakiwachochea wafanyakazi wameambulia patupu kwani wafanyakazi daima wako pamoja na mfumo na Mapinduzi ya Kiislamu.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*