?>

Korea Kaskazini yatangaza hali ya hatari baada ya COVID-19 kuenea

Korea Kaskazini yatangaza hali ya hatari baada ya COVID-19 kuenea

Korea Kaskazini imethibitisha mlipuko wake wa kwanza wa COVID-19 Alhamisi na kutangaza hali ya hatari huku vyombo vya habari vya serikali vikitangaza kuwa COVID-19 aina ya Omicron imegunduliwa katika mji mkuu Pyongyang.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametaka kuimarishwa hatua za kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 kufuatia kutangazwa kisa chake cha kwanza cha maambukizi ya kirusi hicho miaka miwili tangu janga la corona kuanza.

Shirika la habari la Korea  (KCNA) limesema vipimo vilivyofanywa siku ya Alhamisi kutoka kwa watu mbalimbali katika mji mkuu Pyongyang vimethibitisha walikuwa wameambukizwa na aina ya kirusi cha Omicron. Shirika hilo pia limesema Kim aliitisha mkutano wa wakuu wa Chama cha Wafanyakazi cha Korea, ambapo wanachama waliamua kuimarisha hatua za kudhibiti maambukizi ya kirusi hicho.

Korea Kusini imekuwa ikishuku kwa muda mrefu kuwa Korea Kaskazini haitoi ripoti sahihi kuhusu maambukizi ya COVID-19 hasa kwa kuzingatia kuwa ugonjwa huo ulienea sana katika nchi jirani ya China na Korea Kusini yenyewe.

Korea Kaskazini iliweka sheria kali za karantini wakati ugojwa wa COVID-19 ulipotangazwa mapema 2020. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani hadi sasa watu 64,207 kati ya watu milioni 24.7 wamepimwa COVID-19 Korea Kaskazini na hakuna aliyepatikana na ugonjwa huo hadi kufikia Machi 31.

Korea Kaskazini imekataa kupokea chanjo za COVID-19 kutoka nje ya nchi hiyo na haijulikani iwapo nchi hiyo ina chanjo yake yenyewe.

 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*