?>

Kuendelea kugunduliwa makaburi ya umati ya Wahindi Wekundu Canada

Kuendelea kugunduliwa makaburi ya umati ya Wahindi Wekundu Canada

Makaburi ya umati ya Wahindi Wekundu, ambao ni wakaazi asili wa Canada, yangali yanaendelea kugunduliwa nchini humo. Kuhusiana na nukta hiyo Jumanne vyombo vya habari viilitangaza habari ya kugunduliwa kaburi jingine la umati lenye maiti za watoto zaidi ya 160 wa Wahindi Wekundu na wakazi asilia wa Canada katika mkoa wa British Colombia.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika wiki za hivi karibuni, kumepatikana makaburi ya umati ya watoto nchini Canada na hivyo kupelekea  nchi hiyo kuendelea kukabiliwa na lawama za kimataifa. Watoto hao kutoka makabila asili ya Canada waliteganishwa na wazazi wao katika kipindi cha kuanzia mwaka 1890 hadi 1970 na kupelekwa katika shule za bweni ambazo zilikuwa zinasimamiwa na Kanisa Katoliki.

Lengo kuu la kutekelezwa mradi huo lilikuwa ni kuwatenganisha watoto hao na jamii zao asili za Canada ili kuwazuia kujifunza lugha, mila na desturi zao. Watoto hao walikumbwa na masaibu chungu nzima ambapo wengi waliteswa na kunajisiwa na kudhalilishwa kijinsia shuleni. Kutokana na hali hiyo baadhi ya watoto walipoteza maisha msimu wa baridi wakiwa jangwani wakijaribu kutoroka hali mbaya shuleni. 

George Manuel, mmoja kati ya watu ambao walikuwa katika shule hizo katika muongo wa 1920  anasema wanafunzi katika shule hizo pia walikabiliwa na njaa. Aidha anasema katika msimu wa baridi shule hizo hazikuwa na vifaa vya joto na wanafunzi waliishi katika hali duni ya kiafya.

Aidha nyaraka zingine zinaonyesha kuwa watoto hao kutoka jamii asili za Canada pia walikumbwa na magonjwa kama vile surua, homa, kifua kikuu na magonjwa mengine  ya kuambukiza na hawakuwa wakipata matibabu ya kutosha hivyo wengi walipoteza maisha.

Gazeti la Washington Post limeandika kuhusu kadhia hiyo na kubaini kuwa, kugunduliwa makaburi hayo ya umati ni kashfa katika historia ya Canada ambapo mmoja wa viongozi wa jamii asili za Canada ameyataja kuwa, 'hasara isiyoweza kutasawarika"

Baada ya kutangazwa kashfa hizo za kugunduliwa makaburi ya umati ya watoto wa jamii asili za Canada, kumeibuka hitilafu kati ya serikali na Kanisa Katoliki.

Serikali ya Canada ambayo imekuwa ikijinadi kuwa eti ni mtetezi wa haki za binaadamu sasa iko chini ya mashinikizo makali kiasi kwamba Waziri Mkuu wa nchi hiyo Justin Trudeau amekiri kuwa kadhia ya makaburi ya umati ni kumbukumbu ya ukurasa wa kuogofyaa wenye aibu katika historia ya Canada na kwamba ni kashfa kubwa lakini pamoja na hayo amekataa kuomba msamaha.

Justin Trudeau ambaye hivi sasa yuko chini ya mashinikizo ndani ya Canada na pia katika uga wa kimataifa anasisitiza kuwa Kanisa Katoliki ndilo linalopaswa kuwajibishwa kuhusu kashfa ya makaburi hayo ya umati na hivyo, kiongozi wa kanisa hilo, Papa Francis, ndiye anayepaswa kuomba radhi.

Hii ni katika hali ambayo, Papa Francis naye pia hajakubali kuomba radhi hata baada ya kubainika wazi kuwa Kanisa Katoloki lilihusika katika mauaji hayo ya kinyama ya watoto asili wa Canada na badala yake ametaka kuwepo uchunguzi wa pamoja baina ya wakuu wa kanisa na viongozi wa kisiasa. Papa Francis ametosheka tu na kusema anafungamana na wenyeji asili wa Canada kutokana na kasfha hiyo na kwa hivyo naye pia amekataa kuomba radhi.

Kugunduliwa mutawalia makaburi ya umati Canada ni kashfa kubwa kwa serikali ya nchi hiyo ya Amerika Kaskazini na ulimwengu wa Magharibi kwa ujumla.  Ukweli ni kuwa kugunduliwa makaburi hayo ya umati kunaashiria namna ambavyo Wamagharibi ni wabaguzi na jinsi walivyo mbali na nara zao za eti kutetea haki za binadamu. 

Saa Hiil Thut, mwenye umri wa miaka 72 na ambaye alisoma katika shule ya msingi ya bweni ya  Kamloops Indian, ambayo ni kati ya maeneo yaliko makaburi hayo ya umati, anasema hivi kuhusu nukta hiyo: "Hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyewajibishwa kuhusu yaliyojiri katika shule za bweni. Watenda jina wamekwepa mkono wa sheria."

Ni wazi kuwa serikali ya Canada na Kanisa Katoloji zinapuuza kadhia ya haki za binaadamu huku ukweli wa kashfa hii ya makaburi ya umati ukiendelea kubainika. Hakuna shaka kuwa pande hizo mbili hazitaki kukubali au kubeba dhima ya jinai hiyo na hayo yanajiri wakati ambao Canada na nchi za Magharibi zingali zinaendeleza vitendo vya ubaguzi wa rangi na mfano wa hilo ni kubaguliwa wahajiri na watu wasiokuwa wazungu.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*