?>

Kuvunjwa Bunge na mwanzo wa kipindi kipya cha kisiasa nchini Algeria

Kuvunjwa Bunge na mwanzo wa kipindi kipya cha kisiasa nchini Algeria

Katika miaka ya karibuni Algeria imekumbwa na misukosuko na matukio mengi ya kisiasa. Tukio la karibuni kabisa nihatua ya Rais Abdelmadjid Tebboune wa nchi hiyo ya kulivunja Bunge na kuitisha uchaguzi wa mapema. Tebboune alitangaza hatua hiyo Alkhamisi iliyopita katika hotuba yake kwa taifa iliyotolewa kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Taifa ya Shahidi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika hotuba hiyo iliyotangazwa moja kwa moja katika vyombo vya habari, Rais huyo wa Algeria amesema: "Nimechukua uamuzi wa kulivunja Bunge na kuelekea kwenye uchaguzi usiokuwa na ufisadi ambao milango yake itakuwa wazi kwa vijana. Vilevile naazimia kutekeleza matakwa yote ya wananchi kuhusu marekebisho ya Katiba." Abdelmadjid Tebboune ameongeza kuwa, mabadiliko katika baraza la mawaziri yatafanyika katika kipindi cha chini ya masaa 48 yajayo na kwamba mabadiliko hayo yatajumuisha sehemu ambazo wananchi wametaka zifanyiwe marekebisho na utendaji wake umekuwa dhaifu.

Inaonekana kuwa, agizo la kuvunjwa Bunge la Algeria na kuitishwa uchaguzi wa mapema sambamba na kulifanyia marekebisho baraza la mawaziri ni hatua iliyochukuliwa na Rais wa Algeria kwa ajili ya kutimiza matakwa ya wananchi ya kuwepo mapokezano ya uongozi na kushika madaraka wanasiasa vijana. Vilevile hatua hiyo imechukuliwa katika fremu ya kupambana na ufisadi wa kiidara na kifedha uliokita mizizi katika taasisi za serikali ya Algeria. Suala hilo pia linatathminiwa kuwa yumkini likawa katika hatua za kuanzisha anga ya wazi ya kisiasa na kutoa fursa kwa shughuli na harakati za vyama na wanasiasa wa kambi ya upinzani. Sambamba na hayo, Rais Abdelmadjid Tebboune ametangaza kuwa ametoa amri ya kuachiwa huru idadi kadhaa ya vinara wa maandamano ya karibuni nchini Algeria na kwamba 55 hadi 60 kati yao wataachiliwa huru.

Abdelmadjid Tebboune mwenye umri wa miaka 75 alishika madaraka ya kuongoza Algeria kupitia uchaguzi wa kwanza kabisa nchini humo ambao ulifanyika bila ya kuwepo rais wa nchi katika historia ya Algeria baada ya kung'atuka madarakani Abdelaziz Bouteflika kufuatia maandamano makubwa ya wananchi. Tebboune  alikuwa waziri mkuu wa Algeria tangu mwezi Mei mwaka 2017 katika kipindi cha utawala wa Boutefika, hadi aliposhinda kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais Disemba mwaka 2019.

Hali ya kisiasa ya Algeria imekuwa ikiyumbayumba tangu Abdelazizi Boutefkika alipolazimika kuachia madaraka ya nchi Aprili mwaka 2019 kutokana na mashinikizo ya wananchi na jeshi la nchi hiyo. Waalgeria wamekuwa wakiandamana mitaani wakitaka kujiuzulu maafisa wa serikali wa kipindi cha Bouteflika, kuhukumiwa viongozi na wanasiasa mafisadi na kutayarishwa mazingira mazuri ya kushiriki makundi na vyama vyote vya siasa katika masuala muhimu ya kitaifa ukiwemo uchaguzi mkuu. Kwa sababu hiyo tangu tarehe 22 Februari mwaka 2019 Waalgeria wamekuwa wakifanya maandamano katika kila siku ya Ijumaa wakitaka kuondolewa madarakani maafisa na viongozi wa kipindi cha Bouteflika waiosalia uongozini. Waandamanaji hao wanaamini kuwa, uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 12 Disemba 2019 uliomfikisha madarakani Abdelmadjid Tebboune, ulihuisha serikali ya zamani ya nchi hiyo na kuwarejesha madarakani maafisa wa utawala wa Bouteflika.

Ni vyema kuashiria hapa kuwa mawaziri wa zamani wa mambo ya nje, mambo wa ndani na sheria wa serikali ya zamani ya Algeria wameendeea kushikia nafasi hizo katika serikali mpya ya nchi hiyo iliyopasishwa na Bunge Februari 2020 baada ya malumbano na mvutano mkubwa wa kisiasa na kijamii. Kwa utaratibu huo tunaweza kusema kuwa, hakuna mabadiliko yoyote ya kimsingi yaliyofanyika katika ngazi ya baraza la mawaziri, na jambo hili halikubaliwi na wapinzani wa serikali. Sasa inaonekana kuwa, Abdelmadjid Tebboune ameamua kufanya mabadiliko au tuyaite "mapinduzi" kuanzia ngazi za juu za uongozi na kushikilia mwenyewe usukani wa kufanya marekebisho ya kisiasa, na ndani ya asasi za Serikali na Bunge.

Hata hivyo inaonekana kuwa, hatua hizo za Tebboune hazitawaridhisha wapinzani ambao wanataka kufanyike marekebisho makubwa zaidi katika mfumo wa utawala wa Algeria.       

342/Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni