?>

Kuwahamisha Wapalestina kwa nguvu ni jinai dhidi ya binadamu

Kuwahamisha Wapalestina kwa nguvu ni jinai dhidi ya binadamu

Afisa mwandamizi wa Palestina amesema hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina sambamba na kubomoa vijiji katika eneo linalokaliwa kwa mambavu na utawala huo la Ukingo wa Magharibi ni jinai dhidi ya binadamu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Waziri wa Uadilifu wa Palestina Shalaldeh aliyasema hayo Jumatatu katika mkutano na waandishi habari akiwa ameandamana na mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), Karim Khan. Katika kikao hicho, Shalaldeh ametoa wito kwa ICC yenye makao yake The Hague ichunguze jinai hizo za Israel.

Ameongeza kuwa, jamii ya kimataifa, hasa ICC, inapaswa kuchukua hatua za kuwawajibisha wale wote waliotenda jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu huko Palesitna kuanzia waziri mkuu wa Israel hadi mlowezi na askari wa Kizayuni.

Aidha amesema kwa mujibu wa sheria za kimataifa, Wapalestina wana haki ya kupambana kutetea haki zao na kupigania uhuru wao.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*