?>

Kuwaua kigaidi waandishi wa habari, mbinu chafu ya Wazayuni ya kujaribu kuficha jinai zake

Kuwaua kigaidi waandishi wa habari, mbinu chafu ya Wazayuni ya kujaribu kuficha jinai zake

Mapema jana Jumatano, mwandishi wa habari ya televisheni ya al Jazeera, Shireen Abu Akleh, 51, alipigwa risasi na kuuliwa shahidi kwa damu baridi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wakati akiwa kwenye kazi yake ya kuripoti uvamizi wa kijeshi wa jeshi la Israel katika kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Jenin.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ali al Samoudi, mwandishi wa gazeti la al Quds la Palestina naye alipigwa risasi kwa nyuma na kujeruhiwa na wanajeshi hao makatili wa Israel.

Katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni umefanya jinai kubwa dhidi ya Wapalestina na kiwango cha jinai hizo kimeongezeka sana hivi sasa. Makumi ya Wapalestina wameuawa shahidi na mamia ya wengine wameshajeruhiwa. Katika kuendeleza jinai zake dhidi ya Wapalestina, utawala wa Kizayuni unakanyaga kijeuri na wazi wazi kabisa haki za kidini na za kuishi za Wapalestina na wakati wowote Waislamu wanapolalamikia kuvamiwa Msikiti wa al Aqsa na Wazaayuni, wanajeshi makatili wa Israel hutumia nguvu kupita kiasi kuwakandamiza Waislamu hao na kupiga mabomu ndani ya Msikiti huo ambao ndicho Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

Ijapokuwa vyombo vingi vya habari vya Magharibi na vya Kiarabu vinapenda kunyamazia kimya jinai zinazofanywa na Wazayuni dhidi ya Wapalestina, lakini utawala huo dhalimu unashindwa kuvumilia hata ripoti za chini kabisa za kufichua jinai zao. Shireen Abu Akleh alikuwa ripota wa zamani zaidi na mashuhuri zaidi wa kike wa televisheni ya al Jazeera. Amepata umaarufu mkubwa katika matukio ya Palestina. Mwandishi huyo amepigwa risasi kichwani na kwa makusudi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wakati alipokuwa anaandaa ripoti kuhusu uvamizi wa wanajeshi wa Israel katika kambi ya Jenin, ya wakimbizi ya Kipalestina. Jinai hiyo inazidi kudhihirisha kiwango kikubwa mno cha ukatili wa utawala wa Kizayuni ambao kwake kuua wanadamu ni jambo rahisi mno.

Hii si mara ya kwanza kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kutenda jinai kama hiyo. Kabla ya hapo, utawala huo katili umetenda jinai nyingi tu dhidi ya waandishi wa habari. Lengo la jinai hizo za Israel ni kujaribu kuzuia kuripotiwa ukatili na jinai zake inazowafanyia Wapalestina na raia wasio na ulinzi. Ukweli ni kuwa, utawala wa Kizayuni unafanya jinai za kuwaua kigaidi waandishi wa habari ili kuwazuia wasiakisi wala kufichua ukatili mkubwa wanaofanyiwa wananchi wasio na ulinzi wa Palestina. Ni kwa sababu hiyo ndio maana televisheni ya al Jazeera aliyokuwa akiripotia Bi Shireen Abu Akleh ikatangaza kuwa, jinai hiyo ya kutisha imevunja sheria za kimataifa na lengo lake ni kukanyaga uhuru wa vyombo vya habari unaotambuliwa kimataifa.


342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*