?>

Lavrov: Maombi ya nchi za Ulaya ya kununua chanjo ya corona ya Russia yanazidi kuongezeka

Lavrov: Maombi ya nchi za Ulaya ya kununua chanjo ya corona ya Russia yanazidi kuongezeka

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameitaja chanjo ya Sputnik- V kuwa moja ya chanjo bora zilizopo duniani hivi sasa na kusisitiza kuwa, maombi ya nchi za Ulaya ya kununua chanjo hiyo yanazidi kuongezeka.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sergei Lavrov amekosoa mwenendo wa Umoja wa Ulaya na kueleza kuwa, muundo wa Umoja wa Ulaya uko kwa namna kwamba hauruhusu kuwepo ushirikiano huru baina ya umoja huo na Russia katika suala la chanjo ya corona. 

Lavrov ameongeza kuwa, kwa hali yoyote ile kinachojadiliwa ni kuwa, ni nani atachukua hatua ili kuzuia  japo kidogo kuvurugika uhusiano  kati ya Moscow na Brussels.  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameongeza kuwa, leo hii nchi nyingi kama Jamhuri ya Czech zinasubiri kuidhinishwa chanjo ya Sputnik-V na taasisi ya madawa ya Umoja wa Ulaya ili kuweza kuiagiza. Huko Hungary pia hivi sasa wanaifuatilia chanjo hiyo na wametangaza kuwa tayari kuinunua. Wakati huo huo maombi ya nchi za Ulaya ya kununua chanjo hiyo ya Russia yanazidi kuongezeka. Ni siku kadhaa tu zilizopita pia sisi tulipokea ombi kutoka kwa Mfalme wa Monaco akitaka kupatiwa chanjo jamii nzima ya nchi hiyo ndogo inayopatikana katika pwani ya bahari ya Mediterania. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni