?>

Lavrov: Vikwazo vya Magharibi haviwezi kuvunja irada ya wananchi wa Russia

Lavrov: Vikwazo vya Magharibi haviwezi kuvunja irada ya wananchi wa Russia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov amesema, vikwazo vya Magharibi havina athari yoyote mbele ya irada ya watu wa nchi hiyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Baada ya Russia kuanzisha operesheni ya kijeshi ndani ya ardhi ya Ukraine mnamo tarehe 24 Februari 2022, Marekani na nchi zingine za Magharibi zilianza kuiwekea Moscow vikwazo vikubwa vya kiuchumi, kama hatua ya kukabiliana na mashambulio ya kijeshi ya nchi hiyo dhidi ya Ukraine.

Vikwazo hivyo vimewekwa huku Magharibi ikiwa inachelea kuwa kushadidisha vikwazo dhidi ya Russia katika sekta ya uchumi hasa mafuta na gesi kutaathiri na kuvuruga zaidi hali ya uchumi ya Ulaya na masoko ya nishati duniani.

Vikwazo mbalimbali ilivyowekewa Russia hadi sasa vimeibua changamoto nyingi kwa uchumi wa nchi za Ulaya.

Shirika la habari la TASS limemnukuu waziri wa mambo ya nje wa Russia akisisitiza kuwa, hakuna adhabu wala vikwazo vyovyote vile vitakavyoweza kuvunja irada ya watu wa Russia ya kutetea ukweli wa historia na maslahi ya kisheria ya nchi yao.

Lavrov, ambaye alikuwa anahutubia hafla ya wastaafu wa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo amesema, karibu nchi zote duniani zinatilia mkazo kuwepo kwa nidhamu ya kiuadilifu duniani na akasisitiza: "juhudi tunazofanya sisi si sawa na sheria zilizobuniwa na Marekani ambazo inataka kuzitwisha nchi zingine; bali zinafanyika kulingana na Hati ya Umoja wa Mataifa; taasisi ambayo iliasisiwa baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amebainisha kuwa, watu wasiokubali usawa, ambao wanataka kuitawala dunia wanafanya kila njia ili kuyaandika upya malengo matukufu ya uadilifu na usawa wa kujitawala katika nchi zote.../ 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*