?>

Lavrov: Wamagharibi ndio wanaovuruga utulivu Asia na Afrika Kaskazini

Lavrov: Wamagharibi ndio wanaovuruga utulivu Asia na Afrika Kaskazini

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kwamba nchi yake inaendelea kuisaidia kila upande Libya na kusisitiza kuwa, uvamizi na sisa za kibeberu za nchi za Magharibi ndizo zinazovuruga usalama wa Asia Magharibi na Afrika Kaskazini.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sergey Lavrov alisema hayo jana (Jumatano) wakati alipoonana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya, Mohamed al Taher Siala na kuongeza kuwa, Russia iko tayari kufanya juhudi zake zote kuhakikisha kuwa Libya inafikia kwenye mapatano ya kudumu ya kitaifa na kurejea katika hali yake ya kawaida.

Amezishutumu nchi za Magharibi kwa siasa zao za kibeberu na kuongeza kuwa, eneo la Asia Magharibi limebakishwa nyuma kimaendeleo kutokana na siasa za madola ya Magharibi ambazo zimechochea na kushtadisha mashambulio ya kigaidi katika eneo hilo na kaskazini mwa Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia aidha amesema, mchakato wa kuitatua kisiasa kadhia ya Palestina umeingia hatarini kutokana na siasa hizo hizo za madola ya Magharibi.

Itakumbukwa kuwa, jeshi la nchi za Magharibi la NATO liliivamia kijeshi Libya mwaka 2011 na kufanya mashambulio ya chuki, ya kiholela na ya kikatili, yaliyosambaratisha miundombinu kila upande na baadaye nchi hizo za Magharibi ziliitelekeza nchi hiyo huku zikiacha silaha za kila namna zikiwa zimezagaa mikononi mwa makundi hasimu. Matokeo yake hadi leo hii Libya haijawahi kuwa na utulivu unaotakiwa.

Nchi hizo za Magharibi ndizo zilizoanzisha magenge ya kigaidi kama Daesh (ISIS) yenye historia ya kufanya jinai kubwa katika nchi za Waislamu za Asia Magharibi na kaskazini mwa Afrika.

Nchi hizo za kibeberu ni waungaji mkono wakuu pia wa tawala vibaraka katika eneo hili na utawala wa Kizayuni wa Israel unaofanya jinai za kila namna ndani na nje ya Palestina. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni