?>

Lebanon yakumbwa na maandamano baada ya Saad Hariri kujitoa katika jukumu la kuunda serikali

Lebanon yakumbwa na maandamano baada ya Saad Hariri kujitoa katika jukumu la kuunda serikali

Maandamano makubwa yameshuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya Lebanon masaa machache tu baada ya Waziri Mkuu Saad Hariri kutangaza kujiuzulu na kuacha jukumu alilopatiwa na kuunda serikali mpya ya nchi hiyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Maelfu ya wananchi wa Lebanon walijitokeza jana usiku na kuandamana baada ya tangazo la Saad Hariri la kujiondoa na kuachia ngazi jukumu alilopewa na Rais la kuunda baraza la mawaziri. Waandamanaji hao wakilalamikia hatua hiyo ya Saad Hariri walifunga barabara nyingi katika miji muhimu ya nchi hiyo.

Aidha vikosi vya usalama vilivyojitokeza kukabiliana na waandamanaji hao kwa ajili ya kuwatawanya viliandamwa kwa mashambulio ya mawe na waandamanaji hao.

Saad Hariri amejiuzulu ambapo sambamba na kumnyooshea kidole cha lawama Rais Michel Aoun kama aliyekwamishha kuundwa kwa serikali amesema kuwa, mrengo wao katika Bunge la Lebanon hautampendekeza mwanasiasa kwa ajili ya kuwania nafasi ya Waziri Mkuu.

Wakati huo huo, Rais Michel Aoun wa Lebanon amekadhibisha madai hayo na kueleza kwamba, Saad al-Hariri hakuwa tayari kufanya mazungumzo ya aina yoyote yale kwa ajili ya kufanyika mabadiliko katika orodha aliyowasilisha ya mawaziri.

Tangu mwishoni mwa mwaka 2019 na baada ya mripuko uliotokea kwenye bandari ya Beirut, Lebanon imekumbwa na mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa na ughali wa maisha, ongezeko ambalo halijawahi kushuhudiwa la kiwango cha umasikini na mgogoro mkubwa wa kiuchumi. Hali hiyo imeshtadi kutokana na waziri mkuu Hariri kuchelewa kuunda serikali mpya katika anga iliyogubikwa na baadhi ya tofauti za kisiasa

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*