?>

Lebanon yaushtaki utawala wa Kizayuni katika Baraza la Usalama la UN

Lebanon yaushtaki utawala wa Kizayuni katika Baraza la Usalama la UN

Wizara ya Mambo ya Nje ya Lebanon imewasilisha shtaka dhidi ya utawala haramu wa Israel katika Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo kutokana na hatua ya Israel kukiuka mara kwa mara anga ya Lebanon.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Wizara ya Mambo ya Nje ya Lebanon imetangaza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukikiuka mara kwa mara anga ya nchi hiyo katika ukiukwaji wa wazi wa azimio 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.  Lebanon inasisitiza kuwa ukiukwaji huo unapaswa kulaaniwa na usitishwe mara moja ili kudumisha uthabiti na usalama katika eneo.

Rais wa Lebanon Michel Aoun ndiye aliyeamuru wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo iwasilishe malalamiko dhidi ya utawala wa Israel na kusema yakabidhiwe Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipasishwa baada ya kumalizika vita vya siku 33 vya Israel dhidi ya Lebanon mwaka 2006. Azimio hilo liliutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kuchukua hatua dhidi ya Lebanon. Pamoja na hayo utawala huo dhalimu umekuwa ukipuuza azimio hilo kwa kukikiuka anga, nchi kavu, na bahari ya Lebanon.

Lebanon daima imekuwa ikiitaka jamii ya kimataifa iuonye na iukataze utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu ukiukwaji huo wa mamlaka yake ya kujitawala.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni