?>

Maafisa wa Intelijensia wa Saudia wakutana na Rais Bashar al Assad wa Syria

Maafisa wa Intelijensia wa Saudia wakutana na Rais Bashar al Assad wa Syria

Duru za habari zimeripoti kuwa ujumbe maalumu wa serikali ya Saudi Arabia umeelekea Syria, ambako umekutana na kufanya mazungumzo na Rais Bashar al Assad wa nchi hiyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa gazeti la Rai al-Youm, ujumbe huo ulioongozwa na mkuu wa idara ya intelijensia ya Saudia Khalid al-Hamidan, umekutana na kufanya mazungumzo na rais wa Syria katika mji mkuu wa nchi hiyo, Damascus.

Mbali na kukutana na kufanya mazungumzo na rais Assad, ujumbe huo wa kiintelijensia wa Riyadh umefanya mazungumzo pia na Meja Jenerali Ali Mamluk, msaidizi wa masuala ya usalama wa rais wa Syria, ambapo pande hizo mbili zimetilia mkazo suala la uhusiano wa nchi mbili.

Katika mazungumzo hayo, pande mbili za Damascus na Riyadh zimekubaliana kwamba, katika hatua ya kwanza kuelekea kuanzishwa tena uhusiano katika nyanja zote, Saudi Arabia ifungue tena ubalozi wake mjini Damascus.

Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Rai al-Youm, ujumbe wa Saudia umewaeleza maafisa wa Syria kwamba nchi hiyo inakaribisha kurejea tena Syria katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na kushiriki katika mkutano ujao wa jumuiya hiyo utakaofanyika nchini Algeria.

Katika kipindi cha muongo mmoja sasa, Saudi Arabia imekuwa mmoja wa waungaji mkono wakubwa wa makundi ya kigaidi na mpinzani mkuu wa serikali halali ya Syria, ikiwa imetumia mabilioni ya dola kwa lengo la kuuangusha mfumo wa utawala wa nchi hiyo.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*