?>

Maandamano ya kutaka Sheikh Zakzaky achiliwe huru yaendelea Nigeria

Maandamano ya kutaka Sheikh Zakzaky achiliwe huru yaendelea Nigeria

Watu wa Nigeira wameendeleza maandamano ya kutaka serikali ya nchi hiyo imuachilie huru Sheikh Ibrahim Zakzaky kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN).

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Maandamano ya hivi karibuni kabisa yalifanyika Jumatatu katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, ambapo waandamanaji walisikika wakitoa nara za kulaani kuendelea kushikiliwa kinyume cha sheria Sheikh Zakzaky na mke wake.

Walioshiriki katika maandamano hayo, wakiwemo wanawake na vijana walikuwa wamebeba picha za Sheikh Zakzaki huku wakitangaza kumuunga mkono. 

Wafuasi wa Allamah Zakzaky wamekuwa wakifanya maandamano ya amani kwa nyakati tofauti tangu baada ya maafa ya Zaria mwaka 2015. Wafuasi hao wa Sheikh Zakzaky wametaka kuachiwa huru kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na mkewe bila ya masharti yoyote.   

Mwaka 2015 jeshi la Nigeria liliwavamia shughuli za kidini katika Husseiniya ya Imamu wa Zama, katika mji wa Zaria na kuua karibu wafuasi elfu mbili wa Sheikh Zakaky waliokuwa wamekusanyika katika eneo hilo la ibada. Baada ya kumjeruhi Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe, wanajeshi wa Nigeria walimpeleka kusikojulikana. 

Sheikh Zakzaky alijeruhiwa vibaya katika hujuma hiyo ya mashambulizi ya wanajeshi wa Nigeria huko Zaria na hadi sasa jicho lake moja halioni huku lingine likikaribia kupoteza uwezo wa kuona. 

Serikali ya Nigeria imekuwa ikikandamiza maandamano ya wananchi wanaotaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*