?>

Maandamano ya wananchi wa Myanmar ya kukataaa utawala wa kijeshi yaendelea

Maandamano ya wananchi wa Myanmar ya kukataaa utawala wa kijeshi yaendelea

Vyombo vya usalama nchini Myanmar vimewafyatulia risasi waandamanaji wanaopinga jeshi kutwaa madara ya nchi na kuwaua watano miongoni mwao hapo jana Jumapili.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Waandaaji wa maandamano hayo wamenukuliwa wakisema kuwa, wanataka kuutikisa ulimwengu kwa sauti ya umoja ya wananchi wa Myanmar wanaotaka demokrasia kuchukua mkondo wake.

Maandamano hayo yaliyofanyika katika miji mbalimbali ya nchi hiyo jana yalishuhudia vikosi vya usalama vikiwaua kwa risasi raia wawili katika mji wa Wetlet, watu wengine wawili wakiuawa katika mji wa Shan na mwingine mmoja akiuawa kwa risasi pia katika mji wa Hpakant.

Katika mji wa Yangon raia wengi walionekana wakilalamikia utawala wa kijeshi na mauaji yaliyofanywa na vikosi vya usalama kwa kuwasha mishumaa.

Maandamano ya wananchi hao sasa yameingia katika mwezi wake wa nne tangu yalipoanza mwezi Februari kupinga hatua ya kijeshi ya kutwaa madaraka ya nchi hiyo kinyume cha sheria.

Jeshi la Myanmar lilitwaa madaraka ya nchi Februari Mosi mwaka huu baada ya kumkamata Rais wa nchi hiyo, Win Myint na viongozi wengine akiwemo Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama tawala mwenye ushawishi mkubwa, kufuatia siku kadhaa za mivutano nchini humo.

Kisingizio cha jeshi cha kufanya mapinduzi hayo ni madai yake ya kutokea wizi na udanganyifu katika zoezi la uchaguzi wa Bunge wa Novemba mwaka jana (2020), ambapo kwa mujibu wa matokeo, chama tawala cha National League for Democracy (NLD) kinachoongozwa na Aung San Suu Kyi kiliibuka na ushindi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*